Na Dina Ismail, Dar es Salaam
SIMBA SC imeanza maisha mapya chini ya kocha mpya, Mcroatia, Zdravko Lugarusic aliyeanza kuinoa timu jana akirithi mikoba ya Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden’, aliyefukuzwa baada ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Bara mwezi uliopita.
Mwalimu huyo aliongoza mazoezi ya timu hiyo kwa mara ya kwanza jana Uwanja wa Kinesi, Dar es Salaam na miongoni mwa wachezaji waliohudhuria ni kipa mpya, Yaw Beko kutoka Ghana.
Berko aliyewahi kuidakia Yanga SC alisani Mkataba wa miezi sita siku moja na Lugarusic, jana mbele ya Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe.
Berko aliyewahi kuidakia Yanga SC alisani Mkataba wa miezi sita siku moja na Lugarusic, jana mbele ya Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe.

.png)
0 comments:
Post a Comment