Na Majuto Omar, Dar es Salaam
WACHEZAJI wa zamani wa timu taifa ya Tanzania Bara, Tanzania All Stars wako tayari kwa mechi na wenzao wa Kenya, Wazee wa Kazi itakauofanyika mjini Nairobi, Kenya siku ya fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kari, CECAFGA Challenge Desemba 12, mwaka hu.
Nyota wa zamani wa Yanga, Kitwana ‘Popat’ Manara amesema leo kwamba mechi hiyo ya kihistoria imebarikiwa na Baraza la Vyama la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) na wameanza mazoezi makali chini ya usimamizi wake. Timu hiyo inatarajiwa kuondoka Dar es Salaam Desemba 10.
Mbali ya Manara, mchezaji wa zamani wa Simba, Talib Hilal naye anasimamia mazoezi ya timu hiyo yanayofanyika kila siku jioni kwenye viwanja vya Leaders Club jijini. Manara alisema kuwa wapo katika mazoezi ya kina kwa ajili ya mechi hiyo ambayo itachezwa kabla ya fainali ya mashindano hayo.
Alisema kuwa wachezaji wote wapo vizuri na malengo yao ni kuonyesha ubora na vipaji vilivyotukuka walivyokuwa enzi ya ujana wao na kuleta sifa kubwa katika soka laTanzania. Mbali ya Manara, wachezaji wengine wanaounda timu hiyo ni Isihaka Hassan, Mohamed Mkweche, Lawrence Mwalusako, David Mwakalebela, John Mwansasu, Ali Yusuph Tigana, Sekilojo Chambua na Rashid Idd Chama.
Wengine ni Edibily Lunyamila, Mohamed Hussein Mmachinga, Khalid Abeid, James Kisaka, Omari Gumbo. Kutoka Zanzibar ni golikipa Gopi na Mwinyi Bwanga. Alisema kuwa wanatarajia kumjumuisha kipa nyota wa zamani, Juma ‘Mensah’ Pondamali ambaye kwa sasa yupo na timu ya Tanzania Bara, Kilimajaro Stars inayoshiriki mashindano hayo. Kwa upande wa viongozi ni Hassan Mnyenye na mjumbe wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Jamal Lwambo.
“Lengo letu ni kuwa na wachezaji wengi zaidi, lakini wengi wao wameshindwa kujiunga na sisi kutokana na matatizo mbali mbali, hao ndiyo walioitikia wito huo na wameanza mazoezi, tunaomba wadhamini mbali mbali kutusaidia ili kuweza kufanikisha safari hiyo, ni gharama kubwa sana na lengo letu ni kuhamasisha mchezo wa soka, ” alisema Manara.
Huku timu ya Tanzania ikisaka wadhamini, wenzao wa Kenya wanaendelea na mazoezi na wamekwisha taja kikosi kitakacho ikabili timu hiyo. Kikosi hicho kipo chini ya kocha George Sunguti kina wachezaji 30 ambao waliwika Harambee Stars enzi zao.
Wachezaji hao ni makipa James Siang’a, Mohammed Abbas, John Busolo huku mabeki ni , Josphat Murila, Elly Adero, Sammy Pamzo Omollo, Thobias Jua Kali Ochola, Ben Oloo, George Onyango, Wycliffe Anyangu, Paul Ochieng na John Bobby Ogola.
Viungo ni Allan Thigo, Paul Onyiera, ambapo washambuliaji ni Joe Kadenge , Peter Dawo , Ben Musuku, Aggrey Lukoye, J.J Masiga , Mike Amwayi, Douglas Matual, Joe Birgen, Abdul Baraza, Ricky Solomon, James Nandwa, Ambrose Golden Boy Ayoyi, John Nyawaya, David Ochieng’, George Sunguti na Austin Oduor.

![]() |
| KItwana Manara enzi zake akiambaa na mpira dhidi ya mabeki wa Simba SC |

.png)
0 comments:
Post a Comment