• HABARI MPYA

    Monday, December 02, 2013

    CHALLENGE LEO KATIKA PICHA, UGANDA V ERITREA NA SUDAN V RWANDA...

    Mshambuliaji wa Uganda, Emmanuel Okwi kushoto akimtoka beki wa Eritrea, Yonatan Selemon katika mchezo wa Kundi C, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge leo Uwanja wa City, Nairobi, Kenya. Uganda ilishinda 3-0.

    Dan Sserunkuma wa Uganda kulia akigombea mpira na beki wa Eritrea, Yonas Selemun

    Uganda wakishangilia bao lao la kwanza

    Kipa wa Sudan, Abdelrahman Ali akiwa amedaka mpira huku mshambuliaji wa Rwanda,Ndahinduka Michel akiondoka zake katika mchezo wa Kundi C, Kombe la Challenge baina ya timu hizo, Sudan ilishinda 1-0.

    Kipa wa Sudan alikuwa kikwazo kwa Rwanda leo 

    Beki wa Sudan, Malik Mohamed akimdhibiti mshambuliaji wa Rwanda, Ndahinduka Michel

    Kipa wa Sudan aliokolea ndani mpira wa Meddie Kagere kulia aliyeinua mikono, lakini refa akapeta

    Ndahinduka Michel akipmbana katikati ya mabeki wa Sudan

    Ndahinduka Michel akimiliki mpira mbele ya beki wa Sudan

    Winga wa Rwanda, Mugabo Cyza Hussein akimtoka beki wa Sudan, Amier Kamal

    Nahodha wa Rwanda, Haruna Niyonzima akienda chini baada ya kupamiwa na mchezaji wa Sudan, Nadir Eltayeb

    Mpande Joseph wa Uganda kushoto akigombea mpira na beki wa Eritrea, Yonas Selemun

    Dan Sserunkuma kushoto leo alikuwa mwiba na akashinda tuzo ya mchezaji bora wa mechi

    Beki wa Ugand, Wakiro Nico Wadada akipanda kusaidia mashambulizi

    Hamisi Kiiza akitenga mpira apige penalti

    Dan Sserunkuma anapeperuka

    Kocha wa Tanzania Bara, Mdenmark Kim Poulsen kulia na Ofisa wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Iddi Mshangama walikuwepo Uwanja wa City leo 

    Kocha wa Uganda, Mserbia Milutin Sredojevic 'Micho' katikati akizungumza na mshambuliaji wake, Hamisi Kiiza kulia kabla ya mechi. Kushoto ni Kocha Msaidizi, Kefa Kasala. 

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CHALLENGE LEO KATIKA PICHA, UGANDA V ERITREA NA SUDAN V RWANDA... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top