• HABARI MPYA

    Tuesday, November 27, 2012

    AKINA KIIZA, OKWI WANA KAZI NA ETHIOPIA LEO


    Kikosi cha Uganda
    Na Mahmoud Zubeiry, Kampala
    MICHUANO ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge inatarajiwa kuendelea leo kwa michezo miwili ya Kundi A, kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole mjini hapa.
    Wenyeji na mabingwa watetezi, Uganda, The Cranes watashuka dimbani saa 12:00 jioni kumenyana na Ethiopia, mchezo ambao utatanguliwa na mechi kati ya Sudan Kusini na Kenya, Harambee Stars, utakaoanza saa 9:00 Alasiri.
    Mechi zote mbili zinatarajiwa kuwa kali na za kusisimua, kulingana na matokeo ya awali ya mechi za Kundi hilo.
    Cranes iliilaza 1-0 Kenya katika mchezo wa ufunguzi, bao pekee la mshambuliaji wa Saigon Xuan Thanh ya Vietnam, Geoffrey Kizito dakika ya 74, akiunganisha krosi ya Iguma Dennis.
    Ethiopia iliifunga Sudan Kusini 1-0 pia, bao pekee la Yonatal Kebede Teklemariam na kwa matokeo hayo, Korongo wa Kampala wanafungana na Ethiopia kwa kila kitu kwenye Kundi A, kwa pointi tatu na bao moja kila timu. 
    Kenya pamoja na kufungwa walicheza vizuri dhidi ya Uganda na kutengeneza nafasi ambazo walishindwa kuzitumia, wakati wapinzani wao walifanikiwa kutumia nafasi hiyo moja.
    Sudan Kusini walicheza kwa kujihami zaidi siku hiyo, wakimuacha Nahodha wao, Hamisi Leon pekee mbele.
    Wakati mchezo kati ya Uganda na Ethiopia, nchi pekee ya ukanda wa Afrika Mashariki na Kati iliyofuzu Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani nchini Afrika Kusini unatarajiwa kuwa wa pande zote mbili, Kenya wanapewa nafasi kubwa ya kushinda dhidi ya mwanachama mpya wa CECAFA, Sudan Kusini.
    Kikosi cha Uganda leo hakitarajiwi kuwa na mabadiliko makubwa sana na bila shaka kocha Msoctland Bobby Williamson akawarejesha wale wale walioshinda dhidi ya Kenya; Hamza Muwonge, Iguma Dennis, Godfrey Walusimbi,Henry kalungi, Isaac isinde, Hassan Wasswa, Geoffrey Kizito, Moses Oloya, Emmanuel Okwi, Hamisi Kiiza na Brian Umony.
    Kwa Kenya, bila shaka kikosi kitakuwa; Duncan Ochieng, Anthony Kimani, Abdallah Juma, Jockins Atudo, David Owino, David Ochieng, Lama Salim Mohamed, Bernard Wanyama, Humphrey Mieno, Anthony ‘Muki’ Kimani/Enock Obiero na Clifton Miheso/Paul Were.

    MSIMAMO KUNDI A:
     P   W  D   L    GF GA GD Pts
    Ethiopia         1    1    0    0    1    0    1    3
    Uganda          1    1    0    0    1    0    1    3
    Sudan Kusini 1    0    0    1    0    1    -1  0
    Kenya             1    0    0    1    0    1    -1  0

    MSIMAMO KUNDI B:
     P   W  D   L    GF GA GD Pts
    Burundi         1    1    0    0    5    1    4    3
    Tanzania       1    1    0    0    2    0    2    3
    Sudan             1    0    0    1    0    2    -2  0
    Somalia         1    0    0    1    1    5    -4  0

    MSIMAMO KUNDI C:
     P   W  D   L    GF GA GD Pts
    Rwanda         1    1    0    0    2    0    2    3
    Eritrea            1    0    1    0    0    0    0    1
    Zanzibar        1    0    1    0    0    0    0    1
    Malawi          1    0    0    1    0    2    -2  0

    VIWANGO VYA UBORA FIFA
    NCHI                  NAFASI
    Uganda             86
    Malawi              101
    Ethiopia            102
    Sudan                102
    Rwanda             122
    Burundi             128
    Kenya                130
    Tanzania           134
    Zanzibar            134
    Somalia             193
    Eritrea               192
    Sudan Kusini    200
    (Viwango hivi vimetoka mwezi huu)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: AKINA KIIZA, OKWI WANA KAZI NA ETHIOPIA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top