ESS Setif ya Algeria imewasili leo asubuhi Dar es Salaam,
tayari kwa mchezo wao wa kwanza wa Raundi ya Kwanza ya Kombe la Shirikisho
Afrika (CAF) dhidi ya wenyeji, Simba SC mchezo utakaofanyika Jumapili kwenye
Uwanja wa Taifa.
Setif ilitakiwa kufikia katika hoteli ya Durban, Kariakoo
mjini Dar es Salaam- lakini ajabu walifika na kuondoka wakihamia katika hoteli
ambayo hadi jioni hii wenyeji wao Simba SC walikuwa hawajapajua.
Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geoffrey Nyange Kaburu aliiambia
bongostaz kwamba hajajua Setif wamehamia wapi.
Inaoekana Setif wamejipanga kisawasawa, kwani kitendo cha
kufika Dar es Salaam na kuhamia hoteli nyingine bila wenyeji wao kujua si jambo
la mzaha.



.png)
0 comments:
Post a Comment