SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limekipa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa
Morogoro (MRFA) hadi Machi 26 mwaka huu kukamilisha malipo ya sh. milioni 25 ili
kuthibitisha uenyeji wake kwa Fainali ya Tisa Bora ya Ligi Daraja la Kwanza.
MRFA
imeshatanguliza malipo ya sh. milioni 10 kati ya hizo kwa ajili ya kupata kituo
cha fainali ambayo itatoa timu tatu zitakazocheza Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa
2012/2013.
Kwa
hatua hiyo bado mikoa mingine iliyoomba kuwa wenyeji kupitia vyama vyao vya
mpira wa miguu ina fursa ya kuandaa fainali hizo ikiwa itatimiza masharti
yaliyowekwa ikiwemo kulipa kiasi hicho cha fedha (sh. milioni 25).
Kamati
ya Ligi ya TFF itakutana baada ya Machi 26 mwaka huu ili kufanya uamuzi wa
mwisho wa kituo cha fainali hizo zitakazoshirikisha timu tisa.
Timu
zilizofuzu kucheza fainali hizo ni
Polisi ya Dar es Salaam, Mgambo Shooting ya Tanga, Transit Camp ya Dar
es Salaam, Mbeya City Council, Mlale JKT ya Ruvuma, Tanzania Prisons ya Mbeya,
Polisi ya Tabora, Polisi ya Morogoro na Rhino Rangers ya Tabora.
Mikoa
ambayo ilikuwa imeomba tangu awali kuwa mwenyeji wa fainali hizo zilizopangwa
kuanza Machi 31 mwaka huu ni Mbeya, Morogoro, Mwanza, Ruvuma na Tabora.
TFF
iliiandikia mikoa yote kupitia vyama vya mpira wa miguu ikieleza masharti ya
kuwa mwenyeji wa fainali hizo.



.png)
0 comments:
Post a Comment