| Kamati mpya ya Utendaji KRFA |
TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UCHAGUZI
WA VIONGOZI WA
CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU MKOA WA KAGERA (KRFA).
TAREHE 21/03/2012
1.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linawajulisha wadau wa soka kwamba uchaguzi wa
viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa Kagera ulifanyika tarehe 17 Machi
2012, Bukoba mjini kama ulivyokuwa umepangwa.
Uchaguzi huo ulifanyika kwa mujibu wa Katiba ya KRFA na Kanuni za Uchaguzi za
wanachama wa TFF.
2.
Viongozi
waliochaguliwa kwenye Kamati ya Utendaji ya KRFA ni hawa wafuatao:
(i)
Mwenyekiti:
Ndg.
Jamal E. Malinzi
(ii)
Makamu
Mwenyekiti: Ndg.
Alex Raphael Gashaza
(iii)
Katibu
Mkuu: Ndg.
Salum H. Umande
(iv)
Mweka
Hazina: Ndg. Adolf Martin Mahuguli
(v)
Mjumbe
wa Mkutano Mkuu TFF: Ndg. Peregrinius A. Rutayuga
(vi)
Mjumbe-
Mwakilishi wa Vilabu: Ndg. Didas David Zimbihile
(vii)
Wajumbe-
Kamati ya Utendaji: - Ndg. Abubakari Kazinja
- Ndg. Dionise Magezi
- Ndg. Ezekiel Geofrey Samson
3.
TFF
inawashukuru wadau wa soka Mkoani Kagera, hususan, wajumbe wa Mkutano Mkuu wa KRFA
na Kamati ya Uchaguzi ya KRFA kwa kuheshimu na kuzingatia Katiba ya KRFA, Kanuni za Uchaguzi za wanachama wa TFF na kwa
ushirikiano mkubwa walioutoa kwa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, hivyo kufanikisha kufanyika
kwa uchaguzi wa KRFA kama ulivyopangwa. Ni matumaini ya TFF kuwa wadau wa soka
Mkoani Kagera wataendelea kushirikiana na TFF kuendeleza soka katika Mkoa wa Kagera.
Sunday Kayuni
KAIMU KATIBU MKUU


.png)
0 comments:
Post a Comment