• HABARI MPYA

    Wednesday, March 04, 2026

    ULINZI NA USALAMA MICHEZONI NI MIONGONI MWA VIPAUMBELE VYA MAANDALIZI YA AFCON 2027

    KATIKA kuendelea na  maandalizi ya mashindano ya AFCON 2027,  Kamati ya Kitaifa ya mashindano hayo, imeanza kuweka mikakati madhubuti ya  ulinzi na usalama michezoni.
    Hayo yamejiri katika kikao cha kamati hiyo kilipokutana na  Mkuu wa Kitengo cha Usalama Michezo kutoka Umoja wa Mataifa (UN), Bw. Valeroo de Divitiis tarehe 4 Machi, 2026 jijini Dar es Salaam.
    Akizungumza katika kikao hicho, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Boniface  Tamba alisisitiza umuhimu wa kuweka mikakati madhubuti ya ulinzi na usalama itakayohakikisha mashindano ya AFCON 2027 yanafanyika katika mazingira salama, yenye utulivu na yanayokidhi viwango vya kimataifa. Alibainisha kuwa Tanzania ikiwa ni miongoni mwa nchi waandaji, ina wajibu wa kuhakikisha miundombinu ya viwanja, mifumo ya udhibiti wa umati, pamoja na usimamizi wa matukio makubwa ya michezo vinaimarishwa kwa kuzingatia miongozo ya kimataifa.
    Alisema kikao hicho kinalenga  kuimarisha uratibu kati ya taasisi za usalama na michezo, kufanya tathmini ya vihatarishi (risk assessment), pamoja na kuweka mifumo thabiti ya usimamizi wa usalama itakayohakikisha Tanzania inatimiza wajibu wake kama mmoja wa waandaji wa mashindano hayo makubwa barani Afrika.
    Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya AFCON 2027, Bw. Leodgar Chila Tenga alisema dhamira ya Serikali na wadau wa michezo ni  kuhakikisha AFCON 2027 inakuwa mashindano yenye mafanikio makubwa, si tu kwa ubora wa kiufundi wa michezo, bali pia kwa viwango vya juu vya ulinzi na usalama.
    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ULINZI NA USALAMA MICHEZONI NI MIONGONI MWA VIPAUMBELE VYA MAANDALIZI YA AFCON 2027 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top