TIMU ya TRA United imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara mchana wa leo Uwanja wa Black Rhino, Karatu Jijini Arusha.
Mabao ya TRA United, zamani Tabora United yamefungwa na beki Muivory Coast, Chamou Karaboue dakika ya 62 na mshambuliaji Mganda, Joseph Akandwanaho dakika ya 90’+2.
Kwa ushindi huo, TRA United inafikisha pointi 19 katika mchezo wa 14 na kusogea nafasi ya tisa, wakati Namungo FC inabaki na pointi zake 21 za mechi 17 sasa na kushuka kwa nafasi moja hadi ya saba.
Beki wa zamani wa Simba SC na Cote RC Abidjan ya kwao, Iivory Coast, Chamou Karaboue ndiye aliyechaguliwa Mchezaji Bora wa Mechi baada ya mchezo huo.



.png)
0 comments:
Post a Comment