• HABARI MPYA

    Wednesday, February 19, 2020

    TFF YAMTEUA WAZIRI DK. DAMAS NDUMBARO KUWA MWENYEKITI WA KAMATI YA RUFANI NA LESENI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    NAIBU Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Damas Ndumbaro ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Rufani za Leseni ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
    Taarifa ya TFF leo, imesema kwamba Dk. Ndumbaro atasaidiwa na Dk. Alex Mgongolwa, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe Charles Matoke, David Kivembele na Robert Selasela.
    Pamoja na hayo, Kamati ya Utendaji ya TFF imeunda Kamati ya Maendeleo ya Miradi ili kusimamia utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa vituo vya michezo vya Kigamboni, Dar es Salaam na Tanga.

    Naibu Waziri, Dk. Damas Ndumbaro ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Rufani za Leseni ya TFF 

    Kabla ya kuunda Kamati hiyo, Kamati ya Utendaji ilipokea taarifa ya maandalizi ya utekelezaji wa miradi hiyo kwenye kikao chake kilichofanyika Februari 18, 2020 jijini Dar es Salaam.
    Wajumbe wa Kamati hiyo ni QS Lucy Mzengi (Mwenyekiti), Mhandisi Hersi Said, Mhandisi Hamad Ramadhan, na Mhandisi Charles Adrian.
    Kikao hicho cha kawaida vilevile kilipokea Taarifa ya Rais, Taarifa ya Utekelezaji ya Sekretarieti, Utekelezaji wa Mpango Mkakati wa TFF (StrategicPlan) kwa mwaka 2020 na kufanya uteuzi wa Kamati ndogo za TFF.
    Wajumbe walioteuliwa katika Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ni Mwanasheria Elias Mwanjala (Mwenyekiti), Said Soud (Makamu Mwenyekiti), Zakaria Hans Poppe, Issa Batenga, Wakili Msanifu Kondo, na Said George. 
    Kamati ya Fedha na Mipango ni Athumani Nyamlani (Mwenyekiti), Francis Ndulane (Makamu Mwenyekiti), Pascal Kihanga, Maxmillian Tabonwa, Paul Bilabaye, Allen Mrindoko, Evans Mgeusa, na Seif Muba.
    Kamati ya Mashindano ni Ahmed Mgoyi (Mwenyekiti), Saloum Chama (Makamu Mwenyekiti), James Mhagama, Patrick Kahemele, Fortunatus Kalewa, Shafih Dauda, Sarah Chao, Said Tully, na Ali Kamwe. 
    Kamati ya Ufundi ni Vedastus Lufano (Mwenyekiti), Mrisho Bukuku (Makamu Mwenyekiti), Ibrahim Masoud, Ally Mayay, Michael Bundala, Jumbe Menye,na Edibily Lunyamila.
    Kamati ya Mpira wa Vijana ni Khalid Abdallah (Mwenyekiti), Lameck Nyambaya (Makamu Mwenyekiti), Mohamed Aden, Nassib Mabrouk, Salim Kibwana, Vicent Majili, Kenneth Pesambili, Nicky Magarinza, na Philip Alando.
    Kamati ya Waamuzi ni Soud Abdi (Mwenyekiti), Israel Nkongo (Makamu Mwenyekiti), Zahra Mohamed, John Kanyenye, na Samwel Mpenzu.
    Kamati ya Mpira wa Wanawake ni Amina Karuma (Mwenyekiti), Mia Mjengwa (Makamu Mwenyekiti), Rose Kisiwa, Somoe Ng’itu, Zena Chande, Beatrice Mgaya, Sofia Tigalyoma na Zabibu Juma. 
    Kamati ya Habari na Masoko ni Steven Mnguto (Mwenyekiti), Osuri Kosuri(Makamu Mwenyekiti),Cyprian Kuyava, Mgaya Kingoba, Dk. Omar Saleh na Saleh Ally.
    Kamati ya Tiba ni Dk. Paul Marealle (Mwenyekiti), Dk. Fred Limbanga (Makamu Mwenyekiti), Dk. Norman Sabuni, Dk. Lisobina Kisongo, Dk. Eliezer Ndama, Dk. Billy Haonga, na Dk. Violet Lupondo. 
    Kamati ya Futsal na Beach Soccer ni Blassy Kiondo, Isaac Munisi, na Didas Zimbihile.
    Kamati ya Leseni za Klabu ni Wakili Lloyd Nchunga (Mwenyekiti), Wakili Emmanuel Matondo (Makamu Mwenyekiti), Sunday Kayuni, George Mayawa, na Tumaini Mringo. 
    Kamati ya Rufani za Leseni ni Dk. Damas Ndumbaro (Mwenyekiti), Dk. Alex Mgongolwa (Makamu Mwenyekiti), Charles Matoke, David Kivembele, na Robert Selasela.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TFF YAMTEUA WAZIRI DK. DAMAS NDUMBARO KUWA MWENYEKITI WA KAMATI YA RUFANI NA LESENI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top