• HABARI MPYA

    Thursday, February 13, 2020

    REFA ALIYECHEZESHA MECHI YA YANGA SC NA LIPULI FC UWANJA WA TAIFA AFUNGIWA MIEZI MITATU

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    REFA Abubakar Mturo aliyechezesha mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara baina ya wenyeji, Yanga SC na  Lipuli FC ya Iringa Februari 5, mwaka huu Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam amefungiwa miezi mitatu.
    Taarifa ya Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kwa Vyombo vya Habari leo imesema kwamba Mturo amefungiwa kosa la kushindwa kumudu mchezo huo ambao Yanga SC iliibuka na ushindi wa 2-1
    Taarifa hiyo inayofuatia kikao cha Februari 10, imeongeza kwamba adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni namba 39 (1) ya Ligi Kuu Kuhusu Udhibiti wa Waamuzi, ingawa haikuzama ndani kusema kosa lipi refa huyo alifanya siku hiyo.
    Vile vile katika mchezo huo mwamuzi msaidizi namba mbili Joseph Pombe amefungiwa miezi mitatu, kwa kosa la kushindwa kumudu mchezo – naye pia adhabu yake imetolewa kwa kuzingatia Kanuni namba 39(1) ya Ligi Kuu Kuhusu Udhibiti wa Waamuzi.
    Lakini kulikuwa kuna matukio mawili ya utata, ambayo yote yalitokea upande wa refa Msaidizi namba moja, kwanza Yanga kulalamika kunyimwa penalti baada ya Baraka Mtuwi kumchezea rafu mchezaji wao, Mghana Bernard Morrison kwenye boksi aliyekuwa amefanikiwa kumtoka beki mwingine wa Ruvu Shooting, Kassim Simaulanga upande wa kulia.  
    Na lingine ni shuti la mpira wa adhabu lililopigwa na mshambuliaji Paul Nonga, kumsumbua kipa Matecha Mnata hadi wengine kudai aliokolea ndani. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: REFA ALIYECHEZESHA MECHI YA YANGA SC NA LIPULI FC UWANJA WA TAIFA AFUNGIWA MIEZI MITATU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top