• HABARI MPYA

  Tuesday, January 01, 2019

  KMC YAIPIGA 2-0 AFRICAN LYON NA KUJIVUTA JUU KWENYE MSIMAMO WA LIGI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni (KMC) imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya African Lyon katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
  Mabao ya KMC inayofundishwa na kocha Mrundi, Etienne Ndayiragijje ambayo inashiriki Ligi Kuu kwa mara ya kwanza kabisa msimu huu, yamefungwa na Omary Salum aliyejifunga dakika ya 29 na Hassan Kabunda dakika ya 71.
  Kwa ushindi huo, KMC inafikisha pointi 25 baada ya kucheza mechi 19 na kupanda hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu kutoka ya tisa.

  Kwa upande wao, African Lyon kipigo cha leo kinawafanya wabaki na pointi zao 12 baada ya kucheza mechi 18, hivyo kuendelea kukamata nafasi ya 18 kwenye Ligi Kuu ya timu 20.
  Inafuatiwa na Tanzania Prisons yenye pointi 12 pia za mechi 18 na Biashara United yenye pointi 10 za mechi 16. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KMC YAIPIGA 2-0 AFRICAN LYON NA KUJIVUTA JUU KWENYE MSIMAMO WA LIGI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top