• HABARI MPYA

  Wednesday, September 06, 2017

  SALAH AILIPIA KISASI MISRI KWA UGANDA KOMBE LA DUNIA

  MSHAMBULIAJI wa Liverpool, Mohamed Salah jana amefunga bao pekee Misri ikishinda 1-0 dhidi ya Uganda katika mchezo wa Kundi E kufuzu Kombe la Dunia kwa kanda ya Afrika Uwanja wa Alexandria mjini Alexandria.
  Kwa ushindi huo, Misri ambayo haijafuzu Kombe la Dunia tangu mwaka 1990, sasa inaongoza Kundi E ikiwa na pointi tisa baada ya kucheza mechi nne, ikiizidi kwa pointi mbili Uganda.
  Ghana ina pointi tano na bado ina nafasi ya kufuzu, huku Kongo wanaoshika mkia kwa pointi yao moja, wamekwishatolewa. Ikumbukwe ni mshindi wa kundi pekee anafuzu kwa fainali za Urusi mwakani.
  Mohamed Salah jana amefunga bao pekee Misri ikishinda 1-0 dhidi ya Uganda 

  Nyota wa Liverpool, Salah alifunga bao hilo baada ya kuukuta mpira uliorudi dakika ya sita kufuatia shuti la Abdallah Said lililowapita mabeki wa Uganda kupanguliwa na kipa bora Afrika, Denis Onyango.
  Onyango baadaye akaokoa tena michomo mitatu ya haaru kutoka kwa Said na Ramadan Sobhi wakati wageni nao walimtia majaribuni kipa mwenye umri wa miaka 44 wa Misri, Essam El Hadary.
  Kocha wa Misri, Muargentina Hector Cuper atakuwa na matumaini ya kuirudisha Misri kwenye Kombe la Dunia baada ya muda mrefu akishinda mechi dhidi ya Kongo Oktoba 8 nyumbani, kabla ya kuifuata Ghana mwezi Novemba.
  Uganda wao watamenyana na Ghana nyumbani Kampala, Oktoba 7 kabla ya kusafiri kwenda Kongo mwezi Novemba pia.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SALAH AILIPIA KISASI MISRI KWA UGANDA KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top