• HABARI MPYA

    Thursday, September 21, 2017

    RAUNDI YA NNE KOMBE LA LIGI ENGLAND; MAN UNITED NA SWANSEA, ARSENAL, CHELSEA...

    Jose Mourinho wa Manchester United atamenyana na Swansea katika Raundi ya Nne Kombe la Ligi England PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

    RAUND YA NNE CARABAO CUP

    Tottenham v West Ham
    Bristol City v Crystal Palace
    Swansea v Manchester United
    Arsenal v Norwich
    Chelsea v Everton
    Manchester City v Wolves
    Leicester v Leeds
    Bournemouth v Middlesbrough
    Fixtures to be played October 23/24 
    TIMU ya Manchester United itamenyana na Swansea City katika Raundi ya Nne ya Kombe la Ligi England, maarufu kama Carabao Cup. 
    Hiyo inafuatia ushindi wa 4-1 dhidi ya Burton Albion kwenye mchezo wa jana Uwanja wa Old Trafford, mshambuliaji chipukizi, Marcus Rashford akifunga mabao mawili dakika ya tano 17.
    Mabao mengine ya Man United yalifungwa na Jesse Lingard dakika ya 36 na Anthony Martial dakika ya 60, wakati la Burton Albion limefungwa na Lloyd Dyer dakika ya 90 na ushei
    Tottenham watakuwa weneyji wa West Ham mjini London, Chelsea watamenyana na Everton Uwanja wa Stamford Bridge, Arsenal wataikaribisha Norwich na Wolves watamenyana na Manchester City Uwanja wa Etihad.
    Kocha mpya wa Crystal Palace, Roy Hodgson atakwenda ugenini kuifuata Bristol City wakati vinara wa Championship, Leeds watamenyana na Leicester Uwanja wa King Power na mchezo wa mwisho Bournemouth wataikaribisha Middlesbrough.
    Mechi hizo zitachezwa Oktoba 23/24 katika tarehe rasmi  a muda vitakavyotajwa baadaye kwa kila mchezo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RAUNDI YA NNE KOMBE LA LIGI ENGLAND; MAN UNITED NA SWANSEA, ARSENAL, CHELSEA... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top