• HABARI MPYA

    Thursday, September 21, 2017

    SAMATTA, MSUVA NA BANDA WAZIBEBA TIMU ZAO

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    NAHODHA wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta jana amesaidia timu yake, KRC Genk kusonga mbele kwenye mchezo wa Kombe la Ubelgiji baada ya ushindi wa ugenini wa 1-0 dhidi ya Cercle Brugge Uwanja wa Jan Breydelstadion mjini Brugge.
    Bao pekee la Genk jana lilifungwa na kiungo Mspaniola Alejandro Pozuelo Melero dakika ya 18 na baada ya sare ya 0-0 kwenye mchezo wa kwanza nyumbani, Genk sasa inasonga mbele kwa ushindi wa ugenini.  
    Samatta jana alicheza kwa dakika 75, kabla ya kumpisha mshambuliaji kinda wa umri wa miaka 21, Mdenmark, Marcus Ingvartsen.
    Mbwana Samatta (katikati) akiiungana na wenzake kumpongeza mfungaji wa bao la jana, Alejandro Pozuelo Melero 

    Simon Msuva (kushoto) akifurahia na wachezaji wenzake jana nchini Morocco
    Na huo unakuwa mchezo wa 63 kwa Samatta katika mashindano tangu Januari mwaka jana alipojiunga na Genk, kati ya hiyo mechi 36 alianza na mechi 24 ametokea benchi.
    Katika mechi hizo, mshambuliaji huyo wa zamani wa African Lyon, zamani Mbagala Market na Simba zote za Dar e Salaam, amefunga jumla ya mabao 21.
    Kikosi cha Cercle Brugge kilikuwa; Van Damme, Taravel, Vincent, Bruno/Barcelos dk57, Omolo, Robail/Buyl dk80, Gaspar, Imorou, De Belder, Mercier/Tormin dk68 na Sofranac.
    KRC Genk: Vukovic, Mata, Aidoo, Brabec, Khammas, Heynen, Berge, Pozuelo/Malinovskyi dk75, Benson/Buffalo dk85, Writers na Samatta/Ingvartsen dk75.
    Mapema jana, mchezaji mwingine wa Tanzania anayecheza nje, beki Abdi Banda aliisaidia timu yake, Baroka FC kushinda 2-0 ugenini dhidi ya wenyeji, Bloemfontein Celtic katika mchezo wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini, mabao ya Sipho Moeti dakika ya 43 na Gift Motupa dakika ya 87.
    Mchezaji mwingine wa Tanzania, Simon Msuva, usiku wa jana naye ameisaidia timu yake, Difaa Hassan El-Jadida kusonga mbele katika Kombe la FA Morocco baada ya sare ya 1-1 ugenini dhidi ya Ittihad Tanger Uwanja wa Grand Stade de Tanger.
    Msuva aliyejiunga na timu hiyo Julai mwaka huu akitokea Yanga ya nyumbani, alicheza kwa dakika 90 jana na alikuwa ana mchango mkubwa uwanjani. Mchezo wa kwanza hizo zilitoka sare ya 0-0 na jana Difaa imesonga mbele kwa faida ya bao la ugenini.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SAMATTA, MSUVA NA BANDA WAZIBEBA TIMU ZAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top