• HABARI MPYA

    Tuesday, September 12, 2017

    MAJONZI RWANDA, KIPA WA RAYON MUTUYIMANA EVARISTE AFARIKI DUNIA

    Na Canisius Kagabo, KIGALI
    KIPA wa kimataifa wa Rwanda na klabu ya Rayon Sports , Mutuyimana Evariste amefariki dunia jana Jumatatu usiku mjini Kigali, Rwanda.
    Mutuyimana alifariji nyumbani kwake na baada ya hapo mwili wake ukapelekwa kwenye hospitali ya CHUK  kufanyiwa uchunguzi juu ya kifo hicho.
    Kipa huu jana alifanya mazoezi na wenzake siku hiyo na hakuonyesha dalili za tatizo lelote kiafya.
    Lakini vyanzo vinasema kipa huyo amekuwa na kawaida kushikwa na magonjwa ya ghafla na iliwahi kumtokea pia akiwa timu hiyo mjini Dar es Salaam mapema mwezi uliopita kwa ajili ya mchezo wa kirafika dhidi ya Simba SC. 
    Mutuyimana Evariste amefariki dunia jana Jumatatu usiku mjini Kigali, Rwanda 
    Rais wa timu Rayon Sports, Gacinya Chance Denis ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online kwamba magonjwa hayo humshika usiku.
    “Ana kawaida ya kushikwa na magonjwa ya ghafla, yalimshika usiku akiwa mwenyewe nyumbani, tulimpeleka kwenye hospitali, lakini bado kitu kilichosababisha kifo chake hakijajulikana.” Alisema Gacinya alieleza
    Mutuyimana Evariste alijiunga na timu ya Rayon Sports mwaka uliopita kutoka nchini Kenya alipokuwa anachezea Sofapaka.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAJONZI RWANDA, KIPA WA RAYON MUTUYIMANA EVARISTE AFARIKI DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top