• HABARI MPYA

    Tuesday, September 12, 2017

    NE-MO ARUDI KIVINGINE, AACHIA SINGO KALI INAITWA KIPOTABO

    Na Asha Said, DAR ES SALAAM
    MSANII wa  muziki wa kizazi kipya Shaban Mpute 'Ne-Mo' amesema amedhamilia kurudi katika familia ya muziki kivingine, huku akitarajia kuachia wimbo wake mpya unaitwa 'Kipotabo'Septemba 9 mwaka huu.
    Akizungumzia ujio wake huo mpya  Ne-Mo chini ya lebo ya 'Digital City Drimz'  alisema kuwa  amedhamiria kuirejesha RnB ya Bongo katika viwango na pia kuipeleka nje ya mipaka ya Tanzania, kwa sababu anahifahamu vizuri.
    Alisema kwa sasa kuna wasanii kama Diamond Platnumz, Ali Kiba, Vanessa Mdee, Navy Kenzo na wengineo wameubeba muziki wa Bongofleva na kusaidia kuupenyeza kimataifa, naye ana matumaini makubwa ya kufika walipo wasanii hao.
    Msanii Ne-Mo amerudi kivingine na ameachia wimbo wake mpya uitwao Kipotabo 

    Alisema nyimbo yake hii mpya inayokwenda kwa jina la 'Kipotabo' ambayo imetengenezwa katika studio za  Combination Sound  chini ya mtayarishaji Man Water,na video kutengenezwa na Kwetu Studio.
    Ne-mo ujio wake utakuwa wa aina yake na Watanzania hawatajutia kumsubiri Ne-Mo arudi kwa muda wote huo, kwamba ukimya wake umetokana na masomo ambapo aliamua kutulia amalizie masomi kisha aendelee na Harakati za Muziki. 
    Alisema alikuwa masomoni amesomea 'Mass Communication'  anaeleza kuwa sasa ametulia na amepata 'Mameneja '  ambao wanamsimamia na kumrejesha kwa kishindo katika muziki.
    "Nimejipanga vuzri pamoja na mameneja wangu narudi kimuziki kikweli kweli, naomba 
    mashabiki wa muziki Tanzania wanipokee kwa mara nyinyingine, nilitoka kidogo kwenda masomini lakini sasa nimerudi rasmi katika muziki"alisema Ne-mo.
    Alisema kwa upande wa mtindo wa Rap na Hip Hop mwanzoni mwa miaka ya 2000 Profesa Jay alichangia kuuweka muziki wa Hip Hop mtaani na kukubalika na kila kundi la jamii., miaka michache iliyopita waliibuka kina Child Benz na Nako 2 Nako ambao walisaidia kujenga misingi ya kuufanya muziki wa Hip Hop kukubalika kibiashara. 
    Alisema sasa hivi wasanii kama Weusi, Darasa, Billnas, Young Dee na kadhalika ambao wanauwekea vionjo muziki wa Rap kufanya kupenya zaidi na hata uanze kuimbwa na hata akina dada ambao zamani ilikuwa ni nandra kuwa na mapenzi na muziki wa Rap.
    Meneja wa mwanamuziki huyo Habibu Anga 'Guru Picasso' alisema kuwa siku ya Jumatatu wataachia rasmi wimbo wa Kipotabo wa msanii huyo.
    Alisema Ne-mo alikuja kuitikisa zaidi Tanzania na Afrika Mashariki mwaka 2013 alipoanchia wimbo uliokwenda kwa jina la "Number One" ambao alimshirikisha mkali mwenzake 'Ommy Dimpoz' wimbo ambao ulikuwa mkubwa na kugeuka kama 'wimbo wa Taifa' kama wasemavyo mtaani.
    Baada ya mafanikio makubwa ya wimbo huu wa 'Number One' Ne-Mo hakuwahi kutoa kazi 
    yake nyingine yoyote ile, zaidi ya nyimbo za kushikishwa ambazo ni  'Mrs Superstar' ya Young Killer, 'Tulikuwepo' ya Niki Mbishi, 'Sijutii' ya Msamiati na nyinginezo nyingi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NE-MO ARUDI KIVINGINE, AACHIA SINGO KALI INAITWA KIPOTABO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top