• HABARI MPYA

  Sunday, January 01, 2017

  SIMBA KIBARUANI KOMBE LA MAPINDUZI LEO ZENJI

  Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
  MICHUANO ya Kombe la Mapinduzi inaanza rasmi leo kwa mechi mbili za Kundi A kuchezwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Wenyeji KVZ watamenyana na mabingwa watetezi, URA kuanzia Saa 10:00 jioni, kabla ya vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba kumenyana na Taifa Jang'ombe kuanzia Saa 2:30 usiku.
  Mechi za Kundi B zitaanza kesho kwa Azam kucheza na Zimamoto kuanzia Saa 10:00 jioni, kabla ya mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga kumenyana na Jamhuri ya Pemba kuanzia Saa 2:30 usiku. 
  Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog (kushoto) na Msaidizi wake, Jackson Mayanja (kulia)

  Zote Azam, Simba na Yanga ziliondoka Dar es Salaam jana mchana kwenda Zanzibar kushiriki michuano hiyo na zote zimekwenda na vikosi vyao kamili.
  Kikosi cha Simba kilichoondoka jana kinaundwa na makipa: Peter Manyika, Dennis Richard na Daniel Agyei.
  Mabeki ni Hamad Juma, Janvier Bokungu, Novaty Lufunga, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Abdi Banda na Method Mwanjali.
  Viungo ni Said Ndemla, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Mwinyi Kazimoto, Mohammed ‘Mo’ Ibrahim, Muzamil Yassin, James Kotei na washambuliaji Pastory Athanas, Juma Luizio, Mavugo na Blagnon.
  Kikosi cha Yanga kinaundwa na makipa; Deogratius Munishi 'Dida', Benno Kakolanya na Ali Mustafa 'Barthez'.
  Mabeki ni Nadir Haroub 'Cannavaro', Pato Ngonyani, Vincent Andrew, Hassan Kessy, Mwinyi Hajji, Kevin Yondan, Juma Abdul na Oscar Joshua.
  Viungo ni Haruna Niyonzima, Justin Zulu, Simoni Msuva, Juma Mahadhi, Geoffrey Mwashuiya, Deus Kaseke, Saidi Juma 'Makapu', Thabani Kamusoko na Yussuf Mhilu.
  Washambuliaji ni Donald Ngoma, Amisi Tambwe, Emmanuel Martin, Obrey Chirwa na Matheo Anthony. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA KIBARUANI KOMBE LA MAPINDUZI LEO ZENJI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top