• HABARI MPYA

    Wednesday, June 03, 2015

    MZEE YUSSUF WA JAHAZI AWANIA UBUNGE ZANZIBAR

    Na Salum Vuai, ZANZIBAR
    MSANII anayetamba nchini kwa muziki wa taarab za kisasa Mzee Yussuf, anakusudia kujitosa katika ulingo wa siasa kwa kugombea ubunge jimbo la Fuoni, Unguja kupitia Chama cha Mapinduzi.
    Yussuf (pichani) ambaye ni mmiliki na kiongozi wa kundi la Jahazi Modern Taarab na Mjumbe wa zamani wa Kamati ya Utendaji ya Yanga SC, ameambia www.binzubeiry.co.tz jana kwamba sasa wakati wa kutimiza ndoto zake za siku nyingi umefika.
    Msanii huyo alisema licha ya kujaaliwa kipaji cha muziki, lakini kwa miaka mingi amedhamiria kuwa mwanasiasa, na sasa anaanza safari hiyo kwa kuomba ateuliwe kuwania kiti cha ubunge.
    Mbunge mtarajiwa; Mzee Yussuf akiwa amembeba mwimba Taarab mwenzake, khadija 
    kopa

    Kwa sasa nafasi ya ubunge wa jimbo la Fuoni inashikiliwa na Said Mussa Zuberi.
    Alifahamisha kuwa katika siasa hafuati utajiri kwani tayari ameshajijenga vyema kimaisha, na lengo lake kuu ni kutaka kutoa mchango wake katika kuiletea maendeleo zaidi Zanzibar pamoja na wananchi wa jimbo la Fuoni.
    “Kama hali nzuri ya maisha ninayo, umaarufu nimeshapata, sasa naona ni wakati muafaka wa kuwasaidia vijana wenzangu kujikwamua na ugumu wa maisha kwa kushirikiana nao kuibua na kutumia fursa na rasilimali tele zilizopo nchini ili ziwaletee tija,” alibainisha msanii huyo.
    Aidha alisema, pamoja na kutaka kusaidia kuimarisha maendeleo ya Zanzibar kwa jumla, pia iwapo atapata ridhaa ya chama na kuchaguliwa na wananchi, anakusudia kutetea maslahi ya wasanii ili wajengewe mazingira ya kunufaika na kazi zao.
    “Zanzibar imejaaliwa vipaji vingi vya sanaa za aina mbalimbali lakini bado wasanii wa visiwa hivyo hawana maslahi mazuri kama ilivyo katika nchi nyengine,” alieleza Yussuf.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MZEE YUSSUF WA JAHAZI AWANIA UBUNGE ZANZIBAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top