• HABARI MPYA

    Monday, June 22, 2015

    ARSENAL YAIPIGA BAO CHELSEA, YAMSAJILI PETR CECH KWA PAUNI MILIONI 11

    KLABU ya Arsenal imekamilisha usajili ya kipa wa Chelsea, Petr Cech na mlinda mlango huyo anaweza kukutana mapema na klabu yake ya zamani, kwani timu hizo mbili zitamenyana Agosti 2 katika mechi ya Ngao ya Jamii Uwanja wa Wembley.
    Mazungumzo juu ya dili hilo la Pauni Milioni 11 yamekuwa yakiendelea tangu kumalizika kwa msimu ulkiopita na kocha wa Arsenal, Arsene Wenger hatimaye amemnasa kipa huyo mwenye umri wa miaka 33.
    Jose Mourinho alikuwa anasita kumuuza Cech kwa wapinzani wake hao katika Ligi Kuu ya England, na pamoja na taarifa za kukamilika kwa dili hilo, bado hakuna taarifa rasmi zilizotolewa.
    Cech has completed his move from Chelsea to Arsenal ahead of the next  Premier League campaign
    Petr Cech amekamilosha uhamisho wake kutoka Chelsea kwenda Arsenal kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu ya England

    RATIBA YA ARSENAL KWA CECH

    Agosti 2: Ngao ya Jamii vs Chelsea
    Agosti 8: Ligi Kuu vs West Ham (nyumbani)
    Septemba 19: Ligi Kuu vs Chelsea (ugenini)
    Januari 23Ligi Kuu vs Chelsea (nyumbani)
    Paris Saint-Germain inafahamika iliwasilisa maombi rasmi Chelsea kutaka kumnunua kipa huyo wa kimataifa wa Jamhuri ya Czech, ambaye ameamua kubaki London ambako familia yake ipo.
    Cech alitaka mwenyewe kuondoka Chelsea baada ya kupokonywa namba na Mbelgiji Thibaut Courtois katika kikosi cha kwanza cha The Bluse katika msimu ambao timu hiyo ilitwaa ubingwa wa Ligi Kuu na mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich amemfungulia milango ya kutokea.
    Kuwasili kwa Cech The Gunners kunamaanisha mmoja wao kati ya Wojciech Szczesny au David Ospina, ambaye anatakiwa na Fenerbahce, anaweza kuondoka kabla ya msimu mpya.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ARSENAL YAIPIGA BAO CHELSEA, YAMSAJILI PETR CECH KWA PAUNI MILIONI 11 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top