MKONGWE, Xavi ameshindwa kuzuia hisia zake na kumwaga machozi wakati shamrashamra za kumuaga Barcelona kuelekea fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Juventus.
Xavi amemshukuru kocha Luis Enrique kwa kumuwezesha kubaki katika klabu hiyo msimu uliopita.
Kiungo huyo anayeondoka, alitangaza mwezi uliopita kwamba anakwenda kumalizia soka yake katika klabu ya Al-Sadd ya Qatar mwishoni mwa msimu, akihitimisha miaka yake 24 kuwa na vigogo hao wa Katalunya.
Kuelekea fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Juventus, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 alipewa heshima katika klabu ambayo aliitumikia kwa muda mrefu tangu ana umri wa miaka 11 alipojiunga nayo.
Nyota wa Barcelona, Xavi (kushoto) akifuta machozi pembeni ya mchezaji mwenzake, Andres Iniesta wakati shamra shamra za kuagwa Uwanja wa Nou Camp leo PICHA ZAIDI GONGA HAPA


.png)
0 comments:
Post a Comment