• HABARI MPYA

    Wednesday, June 24, 2015

    KWA MTAJI HUU, TUTABADILISHA SANA MAKOCHA!

    RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi jana amemtangaza Charles Boniface Mkwasa kuwa kocha mpya wa timu ya taifa, Taifa Stars akirithi mikoba ya Mholanzi, Mart Nooij aliyeondolewa. 
    Nooij aliyekuwa analipwa dola za Kimarekani 12,500 (zaidi ya Sh. Milioni 25) kwa mwezi, alifukuzwa mwishoni mwa wiki baada ya Taifa Stars kufungwa mabao 3-0 na Uganda Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
    Baada ya mechi 18 jumla za Nooij kuwa mwalimu wa Taifa Stars, ameshinda mechi tatu tu sare sita na kufungwa tisa, timu ikifunga mabao 17 na kufungwa 28. 
    Mkwasa ambaye kwa sasa ni kocha Msaidizi wa Yanga SC, atakuwa akisaidiwa na kocha Hemed Morocco, kocha wa Mafunzo na watafanya kazi kwa kipindi cha miezi mitatu ambayo timu ya taifa itakua na michezo ya kuwania kufuzu kwa CHAN na AFCON.
    Malinzi amesema uteuzi wa makocha hao wazawa umezingatia vigezo vya makocha wa timu ya Taifa kuwa na leseni A ya ukocha kutoka CAF au zinazofanana kutoka mashiriksho mengine duniani wanaozifanyia kazi, jambo ambalo makocha  hao wazawa wamekidhi.
    “Kocha Mkwasa atakua akipewa hudumu zote na masilahi  (zikiwemo posho) alizokuwa anapewa kocha aliyeondoka, pia amepewa nafasi ya kuchagua benchi lake la ufundi la kufanya nalo kazi, hivyo nawaomba wadau wa mpira wa miguu na Watanzania kwa ujumla tuwape sapoti makocha hao wazawa” aliongeza Malinzi”
    Kabla ya mwaka 2006, hali ilikuwa mbaya Taifa Stars kutokana na kutokuwa mdhamini wala utaratibu maalum kuhusu makocha.
    Ni katika kipindi hicho ilishuhudiwa wachezaji wakiwa hawafurahii kuchezea timu ya nchi yao- kutokana na hali mbaya kwa ujumla. Kukaa katika kambi isiyo na hadhi pale Jeshi la Wokovu, huduma mbovu na posho duni, ambazo pia walikuwa wanakopwa.
    Bado viongozi wa TFF tangu enzi za FAT walifanya jitihada za kuunda Kamati za kusimamia timu, zikihusisha wadau mbalimbali wa soka, wengi wao wafanyabiashara maarufu kama Reginald Mengi, Azim Dewji na Mohamed Dewji.
    Mambo yalibadilika mwaka 2006, baada ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuamua kuisaidia timu hiyo na pia kuhamasisha Watanzania kuiunga mkono.
    Rais Kikwete aliamua kubeba jukumu la ajira za makocha wa kigeni na tangu mwaka 2006 timu hiyo imekwishapitia mikononi mwa walimu wanne wa kigeni, kuanzia Mbrazil, Marcio Maximo, Wadenmark, Jan Poulsen na Kim Poulsen na Mholanzi, Mart Nooij.   
    Pamoja na hayo, mwaka wa tisa sasa Tanzania imeshindwa kutimiza ndoto za kushiriki tena Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, ikikosa Fainali tano kuanzia za Ghana 2008, Angola 2010, Gabon na Equatorial Guinea 2012, Afrika Kusini mwaka jana na mwaka huu Equatorial Guinea. 
    Bado hadithi zi zile zile kila siku, wachezaji wetu hawana viwango vya kushindana kimataifa, pamoja na kwamba walimu wa timu za taifa wamekuwa wakipewa fursa nzuri za maandalizi.
    Maximo alipewa kambi mbili za nje ya nchi, Brazil na Ulaya, lakini akaambulia tu kuipeleka timu katika fainali za Ubingwa wa Mataifa Afrika (CHAN), zilizofanyika kwa mara ya kwanza Ivory Coast mwaka 2009. 
    Tangu mwaka 2006, Taifa Stars imekuwa na mdhamini wa kudumu, kuanzia Kampuni ya Bia ya Serengti (SBL) kwa pamoja na benki ya NMB, na sasa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
    Wachezaji wanapewa posho nzuri wanapokuwa kambini na bado Kamati ya Kusaidia timu hiyo nayo imekuwa ikiwapa bakhshishi nzuri hata wanapopoteza michezo, lakini bado matokeo mazuri limekuwa suala gumu. 

    STARS CHINI YA MAXIMO
    KATI ya Juni mwaka 2006 hadi Juni 2010, Taifa Stars ilikuwa chini ya kocha Mbrazil, Marcio Maximo na katia kipindi hicho ilifuzu kucheza Fainali za kwanza za CHAN zilizofanyika Ivory Coast. 
    Huyu ni mwalimu kwanza wa kigeni Taifa Stars tangu kuondoka kwa Mjerumani Burkhad Pape mwaka 2001. 

    REKODI YA MARCIO MAXIMO TAIFA STARS
    P W D L   GF  GA GD Pts
    44 16 15 13 53 48 5 63

    Tanzania 2-1  Burkina Faso (Kufuzu AFCON) Tanzania 0-0 Kenya (Kirafiki)
    Msumbiji 0-0 Tanzania (Kufuzu AFCON) 
    Tanzania 1-1  Angola (Kirafiki) 
    Tanzania 2-0  DRC (Kirafiki)
    Senegal 4-0  Tanzania (Kufuzu AFCON)
    Uganda 1-1  Tanzania (Kirafiki) 
    Tanzania 1-1  Senegal (Kufuzu AFCON) 
    Tanzania 1-1  Zambia (Kirafiki) 
    Burkina Faso 0-1 Tanzania (Kufuzu AFCON)
    Tanzania 1-0  Uganda (Ufunguzi Uwanja wa Taifa) 
    Tanzania 0-1  Msumbiji (Kufuzu AFCON)
    Yemen 2-1  Tanzania (Kirafiki) 
    Tanzania 1-1  Malawi (Kirafiki) 
    Tanzania 1-1  Mauritius (Kufuzu Kombe la Dunia) 
    Cape Verde  1-0  Tanzania (Kufuzu Kombe la Dunia)
    Tanzania 0-0 Cameroon (Kufuzu Kombe la Dunia) 
    Cameroon 2-1  Tanzania (Kufuzu Kombe la Dunia)
    Tanzania 1-1  Ghana (Kirafiki) 
    Mauritius 1-4   Tanzania (Kufuzu Kombe la Dunia)
    Tanzania 3-1  Cape Verde (Kufuzu Kombe la Dunia)  
    Tanzania 1-0 Msumbiji (Kirafiki) 
    Tanzania 0-0 Zimbabwe (Kirafiki) 
    KUFUZU CHAN;
    Kenya 1-2  Tanzania
    Tanzania 1-0 Kenya 
    Tanzania 2-0 Uganda
    Tanzania 1-1  Uganda
    Tanzania  3-1  Sudan
    Sudan 1-2 Tanzania
    22/2/2009: Senegal 1 – 0  Tanzania (CHAN)
    25/2/2009: Tanzania  1 – 0  Ivory Coast (CHAN)
    28/2/2009: Zambia  1 – 1  Tanzania (CHAN)
    09/05/2009: Tanzania 0-2 DRC (Kirafiki) 
    03/06/2009: Tanzania 2-1 New Zealand (Kirafiki) 
    12/08/2009: Rwanda 1-2  Tanzania (Kirafiki) 
    05/11/2009: Misri 5-1 Tanzania (Kirafiki) 
    08/11/2009: Yemen 1-1  Tanzania (Kirafiki) 
    11/11/2009: Yemen 2-1  Tanzania (Kirafiki) 
    Tanzania 0-1  Ivory Coast (Kirafiki) 
    Tanzania 2-3 Uganda (Kirafiki)
    KUFUZU CHAN; 
    Somalia  0-6  Tanzania
    Tanzania 1–1  Rwanda 
    Rwanda  1–0  Tanzania 
    Tanzania 1-5 Brazil (Kirafiki)

    STARS CHINI YA JAN POULSEN
    KATI ya Julai mwaka 2010 hadi Mei 2012, timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ilikuwa chini ya kocha Mdenmark, Jan Borge Poulsen na katika kipindi hicho haikufuzu kucheza Fainali zozote za michuano ya Afrika. 
    Lakini Pouseln akiwa na timu ya Bara, Kilimanjaro Stars aliiwezesha kutwaa Kombe la CECAFA Challenge mwaka 2010 mjini Dar es Salaam. 

    REKODI YA JAN POULSEN STARS
    P W D L   GF GA GD Pts
    22 5 7 10 16 28 -12 22

    Tanzania 1-1 Kenya (Kirafiki) 
    Algeria 1-1 Tanzania (Kufuzu AFCON) 
    Tanzania 0-1  Morocco (Kufuzu AFCON) 
    Misri 5-1  Tanzania (Kombe la Mafuta) 
    Tanzania 1-1 Burundi (Kombe la Mafuta) 
    Uganda 1-1 Tanzania (Kombe la Mafuta) 
    Tanzania 0-2  Sudan (Kombe la Mafuta) 
    Tanzania 1-0 Palestina (Kirafiki) 
    Tanzania 2-1  Jamhuri ya Afrika ya Kati (Kufuzu AFCON)
    Msumbiji  2-0 Tanzania (Kirafiki) 
    Tanzania 0-1  Afrika Kusini (Kirafiki) 
    Jamhuri ya Afrika ya Kati 2-1 Tanzania (Kufuzu AFCON)
    Tanzania 1-1 Algeria (Kufuzu AFCON) 
    Morocco 3-1 Tanzania (Kufuzu AFCON) 
    Chad 1-2  Tanzania (Kufuzu AFCON)
    Tanzania 0-1 Chad (Kufuzu AFCON)
    Tanzania  0-1  Rwanda (Kirafiki) 
    Tanzania 3-0 Djibouti (Kufuzu AFCON) 
    Tanzania 1-2  Zimbabwe (Kirafiki) 
    Tanzania 1-0 Malawi (Kirafiki) 
    Tanzania 0-0 DRC (Kirafiki) 
    Tanzania 1-1 Msumbiji (Kufuzu AFCON)

    STARS CHINI YA KIM POULSEN
    Kuanzia Mei mwaka 2013 hadi Januari 2014, Stars ilihamia mikononi mwa Mdenmark mwingine, Kim Pouslen ambaye alishindwa kuiwezesha timu kucheza Fainali zozote za michuani mikubwa ya kimataifa, iwe CHAN, AFCON hata Kombe la Dunia- au japo kubeba Kombe la Challenge.
    Stars ilifungwa mabao 3-1 na Uganda Uwanja wa Mandela, Namboole mjini Kampala na kufanya kipigo cha jumla cha 4-1 baada ya awali kufungwa 1-0 Dar es Salaam.
    Kime naye akafeli na baada tu ya uongozi mpya wa TFF chini ya Rais Malinzi kuingia madarakani mwishoni mwa mwaka juzi, akaodolewa mwanzini mwa mwaka jana.

    REKODI YA KIM POULSEN STARS
    P W D L   GF GA GD Pts
    30 11 8 11 36 31 5 41

    Tanzania 0 – 0 Malawi (Kirafiki)
    Ivory Coast 2 – 0 Tanzania (Kufuzu Kombe la Dunia)
    Tanzania 2 – 1 Gambia (Kufuzu Kombe la Dunia)
    Msumbiji 1 – 1 Tanzania (Tanzania ilitolewa kwa penalti kufuzu Mataifa ya Afrika)
    Botswana 3 – 3 Tanzania (Kirafiki)
    Tanzania 1-0 Kenya (Kirafiki)
    Tanzania 1-0 Zambia (Kirafiki)
    Tanzania 1-2 Ethiopia (Kirafiki)
    Tanzania 1-0 Cameroon (Kirafiki)
    Tanzania 3-1 Morocco (Kufuzu Kombe la Dunia)
    Sudan 0 – 0 Tanzania (Mechi ya kirafiki Ethiopia)
    Morocco 2-1 Tanzania (Kufuzu Kombe la Dunia)
    Tanzania 2-4 Ivory Coast (Kufuzu Kombe la Dunia)
    Tanzania 0-1 Uganda (Kufuzu CHAN)
    Uganda 3-1 Tanzania (Kufuzu CHAN)
    Gambia 2-0 Tanzania (Kufuzu Kombe la Dunia)
    Tanzania 0-0 Zimbabwe (Kirafiki Dar)
    Namibia 1-1 Tanzania (Kirafiki Windhoek)
    Tanzania  2–0  Sudan (Kundi B Challenge Uganda)
    Tanzania  0–1 Burundi (Kundi B Challenge Uganda)
    Tanzania 7-0 Somalia (Kundi B Challenge Uganda)
    Tanzania 2-0 Rwanda (Robo Fainali Challenge Uganda)
    Tanzania 0–3 Uganda (Nusu Fainali Challenge Uganda)
    Tanzania  1-1 Zanzibar (Mshindi wa tatu Challenge Uganda. Zanzibar ikashinda penalti 6-5) 
    Tanzania 1-1  Zambia (Kundi B Challenge Kenya)
    Tanzania 1-0 Somalia (Kundi B Challenge Kenya)
    Tanzania 1-0   Burundi (Kundi B Challenge Kenya)
    Tanzania 2-2 Uganda (Robo Fainali, Stars ikashinda kwa penalti 3-2 Challenge Kenya)
    Tanzania 0-1 Kenya (Nusu Fainali Challenge Kenya)
    Tanzania 1-1 Zambia (Mshindi wa tatu, Zambia wakashinda kwa penalti Challenge Kenya).

    STARS CHINI YA MART NOOIJ
    Kuanzia Aprili mwaka jana, Taifa Stars imekuwa chini ya Mart Nooij ambaye alikuwa kocha wa nne, baada ya kurejeshwa utamaduni wa kutumia makocha wa kigeni mwaka 2006, tangu mwaka 2001 alipoondolewa Mjerumani, Burkhad Pape.
    Chini ya mzee wetu, Alhaj Muhiddin Ndolanga akiwa Mwenyekiti wa FAT mwaka 2000, aliona Pape hawezi kuwa mtu sahihi kufundisha timu ya taifa katika mwaka wake wa kwanza tu wa kuajiriwa, akamfanya kuwa Mshauri wa Ufundi chini ya makocha Syllersaid Mziray (marehemu) na Mkwasa na timu ikatwaa Kombe la Castle na kufika fainali ya Kombe la Challenge mwaka 2001. 
    Maximo ndiye aliyekuwa wa kwanza wa kigeni akimpokea Mshindo Msolla mwaka 2006, akafuatia Mdenmark, Jan Borge Poulsen mwaka 2010, akafuatia Mdenish mwingine Kim Poulsen aliyemuachia Mart Nooij.
    Makocha wanne Wazungu waliokuwa wanalipwa vizuri- wote wameondoka ndani ya miaka tisa, tulichoambulia ni kucheza CHAN moja kutoka kwa Maximo na Kombe la Challenge tulilopewa na Jan Poulsen mwaka 2010.
    Sasa tunarejea kwa makocha wazalendo na Mkwasa na Morocco wamepewa timu. Jambo zuri na tuwape nafasi.
    Lakini ukweli ni kwamba, wakati umefika sasa tusifanye maamuzi ya jazba kutokana na ghadhabu za matokeo, bali tutafute tatizo la msingi la soka yetu ili tulitafutie suluhisho la kudumu, vinginevyo tutaendelea kubadilisha makocha na hali itabaki kuwa ile ile. 

    REKODI YA MART NOOIJ TAIFA STARS
    P W D L   GF GA GD Pts
    18 3 6 9 17 28 -11 15

    Tanzania 0-0 Malawi (Kirafiki Mbeya)
    Tanzania 1-0 Zimbabwe (kufuzu AFCON Dar es Salaam)
    Tanzania 1-0 Malawi (kirafiki Taifa)
    Tanzania 2-2 Zimbabwe (Kufuzu AFCON Harare)
    Tanzania 2-4 Botswana (kirafiki Harare)
    Tanzania 2-2 Msumbiji (Kufuzu AFCON Dar es Salaam)
    Tanzania 1-2 Msumbiji (Kufuzu AFCON Maputo)
    Tanzania 0-2 Burundi (Kirafiki, Bujumbura)
    Tanzania 4-1 Benin (Kirafiki, Dar es Salaam)
    Tanzania 1-1 Swaziland (Kirafiki, Mbabane)
    Tanzania 1-2 Burundi (Kirafiki, Taifa. Stars Maboresho)
    Tanzania 1-1 Rwanda (kirafiki Mwanza, Maboresho)
    Tanzania 1-1 Malawi (Kirafiki Mwanza, Stars kubwa)
    Tanzania 0-1 Swaziland (COSAFA Rustenburg)
    Tanzania 0-2 Madagascar (COSAFA Rustenburg)
    Tanzania 0-1 Lesotho (COSAFA Rustenburg)
    Tanzania 0-3 Misri (Kufuzu AFCON Alexandria)
    Tanzania 0-3 Uganda (Kufuzu CHAN Zanzibar) 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KWA MTAJI HUU, TUTABADILISHA SANA MAKOCHA! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top