• HABARI MPYA

    Friday, June 26, 2015

    MAKOCHA TIMU ZA VIJANA WAINGIZWA DARASANI LEO

    Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) leo limefungua kozi ya makocha wa mpira wa miguu kwa watoto na vijana kwa nchi nzima kwa lengo la kuhakikisha vijana wengi wanapata nafasi ya kufundishwa mpira na kuucheza mpira kuanzia katika umri mdogo.
    Akifungua kozi hiyo, Katibu Mkuu wa TFF Mwesigwa Selestine amesema ili nchi/Taifa lifanikiwe katika soka ni lazima kuwekeza katika mpira wa watoto na vijana ambao makocha hao ni sehemu ya uwekezaji huo.
    “Tumekua na mashindano ya Taifa U-13, kikosi cha timu ya Taifa ya U-15 ambayo inashirikisha vijana wadogo, vijana hao wanapaswa kupata malezi na mafunzo yenu waalimu ili wafikiapo kuchezea timu za Taifa wawe wamekua kwenye msingi bora wa kuujua mpira wa miguu” alisema Mwesigwa.
    Naye mkufunzi wa FIFA wa kozi hiyo ya makocha kutoka nchini Ujerumani, Eric Muller amesema hata ujerumani imefanikiwa baada ya kuwekeza katika soka la vijana, mwaka 2000 kwenye fainali za Euro nchi yao ilishika nafasi ya mwisho katika msimamo kundi lao kwa kupata poniti moja, lakini uwekezaji walioufanya kwenye soka la watoto na vijana umewapelekea kutwaa Ubingwa wa Dunia mwaka 2014.
    Washiriki wa kozi ya makocha wa timu za vijana za Ligi Kuu

    Washiriki wa kozi hiyo ni makocha wa timu za vijana za mikoa yoye Tanzania, ambao watashirki na timu zao za mikoa katika michuano ya Copa Coca Cola mwaka huu.
    Kozi hiyo ya makocha wa timu za watoto/vijana inayoendeshwa na wakufunzi wa FIFA, Ulric Mathews kutoka shelisheli na Eric Muller kutoka nchini Ujerumani itamalizika jumatatu tarehe 29 Juni, 2015.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAKOCHA TIMU ZA VIJANA WAINGIZWA DARASANI LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top