• HABARI MPYA

    Wednesday, February 12, 2014

    MBEYA CITY NA MTIBWA YAINGIZA MILIONI 25 SOKOINE

    Na Boniphace Wambura, Dar es Salaam
    MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Mbeya City na Mtibwa Sugar iliyochezwa Februari 9 mwaka huu Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya imeingiza sh. 25,602,000.
    Watazamaji 8,534 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo iliyomalizika kwa wenyeji Mbeya City kuibuka na ushindi wa mabao 2-1. Kiingilio katika mechi hiyo kilikuwa sh. 3,000.
    Mgawanyo wa mapato ulikuwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 3,905,389.83, gharama za kuchapa tiketi sh. 489,500 wakati kila klabu ilipata sh. 6,256,097.05.
    Mbeya City inalipa

    Uwanja sh. 3,181,066.52, gharama za mechi sh. 1,908,639.91, Bodi ya Ligi sh. 1,908,639.91, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 954,319.96 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya (MREFA) sh. 742,248.86.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MBEYA CITY NA MTIBWA YAINGIZA MILIONI 25 SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top