Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi amejibu madai ya kwamba anakigeuza chombo hicho kuwa cha watu wa mkoa wa Kagera anakotokea yeye, kwa kulundika watu wengi wa huko kwenye Kamati za shiriksisho hilo.
“Jamani huo sio ukweli, kuna watu zaidi ya 100 sijui kwenye Kamati za TFF, hebu angalieni kuna Wahaya wangapi. Msitake kutengeneza picha kwamba watu fulani hawatakiwi kuwamo ndani ya TFF,”alisema Malinzi alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari leo katika hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro kuhusu siku 100 za kuwapo kwake madarakani TFF.
Malinzi alisema mbona hoja za makabila haziwahi kutokea wakati wa Rais aliyemtangulia, Leodegar Chilla Tenga na akawaasa wadau wa soka kuacha kuleta hila za ukabila kwenye chombo hicho.
Kamati za TFF zinaundwa na Tarimba Abbas, Mwenyekiiti Kamati ya Nidhamu, Wakili Jerome Msemwa (Makamu Mwenyekiti) na Wajumbe Kassim Dau, Nassoro Duduma na Kitwana Manara.
Kamati ya Rufani ya Nidhamu Mwenyekiti Profesa Mgongo Fimbo wakati makamu wake ni Wakili Hamidu Mbwezeleni na Wajumbe ni Titus Bandawe, Twaha Mtengera na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) mstaafu Boniface Mpaze.
Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio ambaye pia kitaaluma ni mwanasheria anaongoza Kamati ya Maadili. Wajumbe ni Wakili Ezekiel Maganja, Wakili Victoria Mandari, Kanali mstaafu Enos Mfuru na Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi, Said Mtanda.
Kamati ya Rufani ya Maadili inaundwa na Jaji mstaafu Stephen Ihema (Mwenyekiti), Wakili Alesia Mbuya (Makamu Mwenyekiti), Lilian Kitomari, Jabir Shekimweri na Chabanga Hassan Dyamwale.
Kabla ya hapo, TFF chini ya rais wake, Jamal Malinzi iliwateua Richard Sinamtwa, Ramadhan Nassib, Dk. Paul Marealle na Saloum Umande Chama kuingia kwenye Kamati ya Utendaji kama Wajumbe wa kuteuliwa.
Kamati ya Fedha na Mipango inaongozwa na Makamu wa Rais wa TFF, Wallace Karia wakati wajumbe ni Francis Ndulane (Makamu Mwenyekiti), Omari Walii, Eliud Mvella, Said Muhammed, Geofrey Nyange, Kidao Wilfred, Ayoub Nyenzi, Lina Kessy na Cyprian Kuhyava.
Geofrey Nyange anaongoza Kamati ya Mashindano wakati wajumbe ni Clement Sanga (Makamu Mwenyekiti), Msafiri Mgoyi, James Mhagama, Mohamed Nassoro, Moses Katabaro, Seif Ahmed, Gerald ambi, Davis Mosha, Said George na Nassoro Idrissa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ni Kidao Wilfred wakati wajumbe ni Athumani Kambi (Makamu Mwenyekiti), Vedstus Lufano, Blassy Kiondo, Rahim Kangezi, Patrick Kahemele, Daud Yassin, Nicholas Mihayo na Dk. Cyprian Maro.
Kamati ya Soka ya Vijana inaongozwa na Ayoub Nyenzi, Khalid Abdallah (Makamu Mwenyekiti), Ali Mayay, Mulamu Ng’hambi, Apollo Kayungi, Said Tully, Luteni Kanali Charles Mbuge, Lameck Nyambaya na Ibrahim Masoud.
Lina Kessy anaongoza Kamati ya Mpira wa Miguu wa Wanawake wakati wajumbe ni Shyrose Bhanji (Makamu Mwenyekiti), Zena Chande, Amima Karuma, Dk. Cecilia Makafu, Zafarani Damoder, Beatrice Mgaya, Sofia Tigalyoma, Martin Mung’ong’o na Engrid Kimaro.
Kamati ya Waamuzi inaongozwa na Saloum Umande Chama, Nassoro Said (Makamu Mwenyekiti), Charles Ndagala (Katibu), Riziki Majala, Kanali Isaro Chacha, Paschal Chiganga, Victor Mwandike, Soud Abdi na Zahra Mohamed.
Hamad Yahya Juma ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi anaongoza Kamati ya Habari na Masoko wakati wajumbe ni Naibu Waziri January Makamba (Makamu Mwenyekiti), Tido Mhando, Yusuf Manji, Yusuf Bakhresa, Samwel Nyalla, Jack Gotham, Fredrick Mwakalebela na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Juma Pinto.
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji inaongozwa na Richard Sinaitwa, Moses Karuwa (Makamu Mwenyekiti), Zacharia Hanspoppe, Hussein Mwamba, Philemon Ntahilaja, Abdul Sauko na Imani Madega.
Kiongozi wa Kamati ya Ukaguzi wa Fedha ni Ramadhan Nassib wakati wajumbe ni Zitto Kabwe (Makamu Mwenyekiti), Nicholas Magarinza, Jackson Songora, Epaphra Swai, Kalilo Samson, Goodluck Moshi, Golden Sanga na Elias Mwanjala.
Dk. Paul Marealle anaongoza Kamati ya Tiba wakati wajumbe ni Dk. Fred Limbanga (Makamu Mwenyekiti), Dk. Mwanandi Mwankemwa, Dk. Nassoro Matuzya, Dk. Eliezer Ndelema na Asha Sadick.
Kamati ya Uchaguzi itakuwa chini ya Mwenyekiti, Wakili Melchesedek Lutema, Makamu wake Wakili Walter Chipeta na Wajumbe Hamidu Mahmoud Omar, Jeremiah John Wambura na Hassan Daalal.
Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF itakuwa chini ya Mwenyekiti Wakili Julius Lugaziya, Makamu wake Wakili Mwita Mwaisaka na Wajumbe Juma Abeid Khamis, Rashid Dilunga na Masoud Issangu, wakati Kamati ya Soka ya Ufukweni iko chini ya Mwenyekiti Ahmed Mgoyi na Wajumbe Deo Lucas, Juma Mgunda, Boniphace Pawasa, Joseph Kanakamfumu na John Mwansasu.
TFF ya Malinzi pia imemuajiri Katibu wa zamani wa klabu ya Yanga SC, Celestine Mwesigwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa shirishiko hilo, wakati katibu wa Simba SC, Wakili Evodius Mtawala ameajiriwa kuwa Mkurugenzi wa Vyama na Masuala ya Kisheria ya TFF na Iddi Mshangama anakaimu ya nafasi ya Mkurugenzi wa Mashindano ya TFF, iliyokuwa inashikiliwa na Saad Kawemba, wakati Danny Msangi atakaimu nafasi ya Mkurugenzi wa Fedha na Utawala TFF na Boniphace Wambura Mgoyo anaendelea kuwa Ofisa Habari wa shirikisho.

![]() |
| Wahaya si haramu TFF; Malinzi katikati akizungumza leo |

.png)
0 comments:
Post a Comment