Na Mahmoud Zubeiry, Nairobi
SUDAN Kusini imekuwa timu ya kwanza kuyaaga rasmi mashindano ya Kombe la
Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge baada ya kufungwa mabao
2-0 na Ethiopia katika mchezo wa Kundi A, uliofanyika Uwanja wa Afrah mjini
Nakuru, Kenya.
Shukrani kwao Yousuf Yassin aliyetokea benchi kipindi cha pili na kufunga
bao la kwanza dakika ya 54 baada ya kupokea pasi nzuri ya Manaye Fantu kutoka
upande wa kulia na Biruk Kalbolre aliyeingia pia ngwe ya pili aliyefunga dakika
ya 82.
![]() |
| Beki wa Sudan Kusini, Clement Badru kushoto akiwa amempiga kwanja mshambuliaji wa Ethiopia, BereketYisak leo Uwanja wa Afrah |
Kwa matokeo hayo, taifa hilo jipya liliojitenga kutoka Sudan, linaaga
mashindano hayo bila kuwa na pointi hata moja, baada ya kufungwa pia mechi zake
mbili za awali, 2-1 dhidi ya Zanzibar na 3-1 na Kenya.
Ethiopia inamaliza kileleni mwa Kundi A kwa pointi zake saba, baada ya
kuwafunga pia na Zanzibar 3-1 na kutoka sare tasa na Kenya.
Mechi ifuatayo baina ya wenyeji Kenya, Harambee Stars na Zanzibar itatoa
mustakabali zaidi wa kundi hilo juu timu
zitakazosonga Robo Fainali.



.png)
0 comments:
Post a Comment