Na Mahmoud Zubeiry, Nairobi
KOCHA wa zamani wa Rwanda, Milutin Sredojevic ‘Micho’ amesema Amavubi inakosa bahati katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashaki na Kati, CECAFA Challenge inayoendelea mjini Nairobi, Kenya ndiyo maana inafanya vibaya.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana baada ya Amavubi kufungwa mechi ya pili mfululizo ya Kundi C, kocha huyo wa Uganda, The Cranes alisema kwamba Rwanda inacheza vizuri lakini inashindwa kupata mabao kwa sababu ya bahati mbaya.
Akasema na mwishowe wanakuja kufungwa bao moja jepesi na mechi inaisha wamelala. “(Uganda) Tumewafunga 1-0 na leo (jana) wanafungwa 1-0 na Sudan, lakini mechi zote wamecheza vizuri na wametengeneza nafasi, ila bahati haikuwa yao,”alisema kocha huyo wa zama ni wa klabu za Villa ya Uganda, St George ya Ethiopia, Orlando Pirates ya Afrika Kusini, E Hilal ya Sudan na Yanga ya Tanzania.
Bao pekee la Salah Ibrahim dakika ya 29 jana, liliipa ushindi wa 1-0 Sudan dhidi ya Rwanda kwenye Uwanja wa nyasi bandia wa City, Nairobi.
Kipigo hicho kinaiweka Rwanda katika mazingira magumu ya kusonga Robo Fainali, baada ya awali pia kufungwa na Uganda 1-0 katika mchezo wao wa kwanza.
Nahodha wa Rwanda, Haruna Niyonzima anayechezea Yanga SC ya Dar es Salaam alijitahidi mno kuwatengenezea nafasi washambuliaji wake, Meddie Kagere na Ndahinduka Michel, lakini walishindwa kuzitumia.
Rwanda sasa itatakiwa kushinda mechi yake ya mwisho na Eritrea kwa mabao mengi na kisha isubiri mustakabali wake wa kwenda Robo Fainali kama moja ya best losers wawili.

![]() |
| RwandaAir inawasubiri; Nahodha wa Amavubi, Haruna Niyonzima alicheza sana jana, lakini wakafungwa 1-0 na Sudan na kocha Micho (pichani chini) amesema wanakosa bahati |
Akasema na mwishowe wanakuja kufungwa bao moja jepesi na mechi inaisha wamelala. “(Uganda) Tumewafunga 1-0 na leo (jana) wanafungwa 1-0 na Sudan, lakini mechi zote wamecheza vizuri na wametengeneza nafasi, ila bahati haikuwa yao,”alisema kocha huyo wa zama ni wa klabu za Villa ya Uganda, St George ya Ethiopia, Orlando Pirates ya Afrika Kusini, E Hilal ya Sudan na Yanga ya Tanzania.
Bao pekee la Salah Ibrahim dakika ya 29 jana, liliipa ushindi wa 1-0 Sudan dhidi ya Rwanda kwenye Uwanja wa nyasi bandia wa City, Nairobi.
Kipigo hicho kinaiweka Rwanda katika mazingira magumu ya kusonga Robo Fainali, baada ya awali pia kufungwa na Uganda 1-0 katika mchezo wao wa kwanza.
Nahodha wa Rwanda, Haruna Niyonzima anayechezea Yanga SC ya Dar es Salaam alijitahidi mno kuwatengenezea nafasi washambuliaji wake, Meddie Kagere na Ndahinduka Michel, lakini walishindwa kuzitumia.
Rwanda sasa itatakiwa kushinda mechi yake ya mwisho na Eritrea kwa mabao mengi na kisha isubiri mustakabali wake wa kwenda Robo Fainali kama moja ya best losers wawili.

.png)
0 comments:
Post a Comment