• HABARI MPYA

    Friday, May 03, 2013

    TFF WAITUMIA DAWA YA KHERI AZAM FC RABAT

    Wachezaji wa Azam wakijifua Rabat

    Na Boniface Wambura
    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) linaitakia kila la kheri timu ya Azam katika mechi yake ya michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika itakayochezwa Morocco kesho (Mei 4 mwaka huu).
    Mechi hiyo ya marudiano ya raundi ya pili ya michuano hiyo itachezwa jijini Rabat kuanzia saa 11 jioni kwa saa za Morocco. Timu hizo zilitoka suluhu katika mechi ya kwanza iliyochezwa jijini Dar es Salaam wiki mbili zilizopita.
    Azam iko nchini Morocco kwa karibu wiki nzima sasa ikijiandaa kwa mechi hiyo chini ya Kocha wake Stewart John Hall. Msafara wa Azam nchini humo unaongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Eliud Mvella.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: TFF WAITUMIA DAWA YA KHERI AZAM FC RABAT Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top