• HABARI MPYA

    Friday, May 24, 2013

    KIEMBA NA KASEJA KUSAINI MIKATABA MIPYA SIMBA SC...NA ITAKUWA MINONOOO

    Juma Kaseja kulia akiwa na kipa mwenzake wa zamani Simba SC, Ally Mustafa Barthez Ikulu mjini Dar es Salaam, ambako timu ya taifa, Taifa Stars ilialikwa na rais Jakaya Kikwete jana.

    Na Mahmoud Zubeiry, IMEWEKWA MEI 24, 2013 SAA 12:05 ASUBUHI
    MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba, Nahodha Juma Kaseja na kiungo Amri Kiemba wamekubali kuongeza mikataba ya kuendelea kuichezea timu hiyo, jambo ambalo ni faraja kwa klabu hiyo.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana, Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Poppe alisema kwamba ni faraja kwa wachezaji hao kukubali kuendelea kuitumikia Simba SC, kwani klabu inaheshimu uwezo na uzoefu wao.
    “Tumesikia kelele nyingi, oooh Kiemba anaenda Yanga, mara oooh Kaseja anakwenda Azam, mimi napenda niwatulize wapenzi na wanachama wa Simba SC, kwamba wachezaji hawa wanabaki Msimbazi.
    “Nimezungumza nao, na wote wamekubali kuongeza mikataba. Tunasubiri warudi kutoka Morocco (wanaenda na timu ya taifa), waje kusaini. Na itakuwa mikataba mizuri tu kwao,”alisema Hans Poppe.
    Kwa upande mwingine, Hans Poppe alisema zoezi la kuwasainisha mikataba mipya wachezaji wote wa timu hiyo linaendelea vizuri, ikiwemo wale waliopandishwa kutoka kikosi cha pili, yaani Simba B.
    Poppe alisema mazungumzo na wachezaji wapya ambao klabu hiyo inawahitaji kuja kuongeza nguvu kikosini, nayo yanaendelea vizuri na kwa umakini na tahadhari ya hali ya juu.
    “Kuna ndugu zetu fulani wao huwa hawajui wachezaji, kwa hiyo kazi yao kutega sikio zao Simba inataka kumsajili nani, basi na wao wanamkimbilia huyo mchezaji na kumsainisha haraka haraka. Kwa hivyo, kwa sasa tunafanya mambo yetu kimya kimya na kwa tahadhari kubwa, hadi tukamilishe ndipo tunamtangaza mchezaji,”alisema.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: KIEMBA NA KASEJA KUSAINI MIKATABA MIPYA SIMBA SC...NA ITAKUWA MINONOOO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top