• HABARI MPYA

    Monday, May 27, 2013

    KUELEKEA TUZO ZA KILI 2013 KIKWETUKWETU, UPI WIMBO BORA WA BONGO POP?


    Na Princess Asia, IMEWEKWA MEI 27, 2013 SAA 5:30 ASUBUHI
    ZOEZI la upigaji wa kura za tuzo za wanamuziki bora Tanzania, maarufu kama Kilimanjaro Music Award lililoanza Mei 2, mwaka huu linazidi kupamba moto kwa wapenzi wa muziki kuwapigia kura wasanii wawapendao.
    Jana kwa muhtasari tulielezea ushindani uliopo katika kipengele cha Wimbo Bora wa Afrika Mashariki ambako Fresh All Day wa Camp Mulla unashindanishwa na Make You Dance wa Keko na Madtrax, Maswali ya Polisi wa DNA, Still A Liar wa Wahu na Valu Valu wa Jose Chameleon.
    Tulijadili hapo tukitoka kujadili ushindani uliopo katika kipengele cha Wimbo Bora wa Reggae ambako Hii Si ya Waiga wa Yuzzo inashindanishwa na Kilimanjaro wa Warriors From The East, Natafuta Paradise wa Mac Malick Simba, Salvation wa Delayla Princess na Tunda wa Hard Mad.
    Awali, tulijadili vipengele vya Wimbo Bora wa Bendi, ambako Chanzo ni Sisi wa Mapacha Watatu unashindanishwa na Jinamizi la Talaka wa Mlimani Park Orchestra ‘Sikinde’, Risasi Kidole wa Mashujaa Band na Shamba la Twanga wa African Stars ‘Twanga Pepeta’ na Rapa Bora wa Bendi ambako Ferguson anachuana na Semsekwa, JS, Jonico na Sauti ya Radi.
    Tulijadili pia kipengele cha Wimbo Bora wenye vionjo vya Asili kinachoshindanisha nyimbo za Aambiwe wa Offside Trick, Atatamani wa AT, Boma la Utete wa Young D, Chocheeni Kuni wa Mrisho Mpoto na Dito na Mdundiko wa Momba na Juma Nature.
    Tulijadili pia Mtayarishaji wa wimbo Bora wa Mwaka kwa bendi, ambako Ababuu Mwana Zanzibar anachuana na Allan Mapigo na Amoroso na Mtayarishaji Chipukizi wa Mwaka, wanakochuana na D Classic, Imma The Boy, Mensen Selecta, Mr T Touch na Sheddy Clever. 
    Tumeangalia pia vipengele vya Mtunzi Bora wa Hip Hop ambako wanaochuana ni Fid Q, Joh Makini, Kala Jeremiah, Mwana FA na Stamina, baada ya juzi kutazama kipengele cha cha Mtunzi Bora wa Mashairi ya Bongo Fleva, tuzo ambayo inashindaniwa na Ally Kiba, Barnaba, Ben Pol, Linex na Ommy Dimpoz.
    Tulitazama vipengele vya Mtunzi Bora wa Mashairi ya Taarab, tuzo inayoshindaniwa na Ahmed Mgeni, Hemed Omary, Khadija Kopa, Mzee Yussuf, na Thabit Abdul, Video ya Wimbo Bora wa mwaka, tuzo inayowaniwa na Ommy Dimpoz kupitia wimbo Baadae, Profesa Jay na Marco Chali wimbo Kamili Gado, Rich Mavoko na wimbo Marry Me, Bob Junior  na wimbo Nichumu na AY na Marco Chali katika wimbo Party Zone na Msanii Anayechipukia tuzo, ambacho tuzo yake inawaniwa na Ally Nipishe, Angel, Bonge la Nyau, Mirror na Vanessa Mdee.
    Msanii Bora wa Hip hop ambacho kinawashindanisha Fid Q, Joh Makini, Kala Jeremiah, Profesa Jay na Stamina na Msanii Bora wa Kiume na wa kike wa Bendi, ambako Kwa wanaume, Chaz Baba anachuana na Dogo Rama, Greyson Semsekwa, Jose Mara na Khaleed Chokora na kwa wanawake Anneth Kushaba anachuana na Luiza Mbutu, Mary Lucos na Vumilia.
    Katika mfulululizo huu, tayari tumejadili vipengele kadhaa vikiwemo vya Msanii Bora wa Kiume na wa Kike Bongo Fleva, ambako kwa wanaume, Ally Kiba anachuana na Ben Pol, Diamond, Linex na Ommy Dimpoz, wakati kwa wanawake Linah anapambana na Mwasiti, Recho na Shaa.
    Msanii Bora wa Kiume na wa Kike Taarabu, ambako Isha Mashauzi, Khadija Kopa, Khadija Yussuf na Leila Rashid wanawania Umalkia na akina Ahmed Mgeni, Hashim Said na Mzee Yussuf wanapigania Ufalme.
    Msanii Bora wa Kiume na wa Kike kwa ujumla, ambavyo vinawashindanisha Ben Pol, Diamond, Linex, Mzee Yussuf na Ommy Dimpoz kwa ‘wakaka’, wakati Isha Mashauzi, Khadija Kopa, Lady Jaydee, Mwasiti na Recho watawania tuzo ya Msanii Bora wa Kike na wimbo bora wa mwaka ambako Rapa Kala Jeremiah, kupitia wimbo wake Dear God anachuana na kundi la Kigoma All Stars na wimbo wao Leka Dutigite, Mwasiti aliyemshirikisha Ally Nipishe katika wimbo Mapito, Ommy Dimpoz aliyemshirikisha Vanessa Mdee katika wimbo Me n U na Ben Pol katika wimbo Pete.
    Leo tunahamia kwenye Wimbo Bora wa Bongo Pop ambako Aifola wa Linex unashindanishwa na Fundi Samuel, Baadae wa Ommy Dimpoz na Angel, Chuki Bure wa marehemu Sharo Milionea na Dully Sykes, Marry Me wa Rich Mavoko na Me n U wa Dimpoz na Vannessa Mdee.  
    Nyimbo zote zilizoingia fainali ni ambazo mwaka jana zilifanya vizuri katika medani ya muziki nchini kiasi cha kujipatia umaarufu mkubwa. 
    Hakika kuna ushindani mkubwa katika vipengele hivi na zaidi wimbo utabebwa na idadi ya kura utakazopigiwa na mashabiki wake ili kushinda tuzo hiyo. 
    Wapiga kura wanatakiwa kuandika namba ya msanii, wimbo, kikundi au bendi anayotaka ishinde na kisha kutuma kwenda namba 15346, wakati njia nyingine zaidi ya ujumbe mfupi (SMS) ni pamoja na Email, kwenda ktma@innovex.co.tz au kutembelea tovuti ya www.kilitimetz.com na kupiga kura moja kwa moja.
    Meneja wa Bia Kilimanjaro Premium Lager, wadhamini wa tuzo hizo, George Kavishe aliiambia BIN ZUBEIRY kwamba, wamejiandaa vizuri mwaka huu kuhakikisha zoezi linafana.
    Kilele cha sherehe za utoaji tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards zilizobeba kaulimbiu ya Kikwetu kwetu ni Juni 8, mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City, ambako pamoja na wasanii mbalimbali kupokea tuzo kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali pia. 
    Je, katika kipengele vya Wimbo Bora wa Bongo Pop, utatoa wapi kura yako?
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: KUELEKEA TUZO ZA KILI 2013 KIKWETUKWETU, UPI WIMBO BORA WA BONGO POP? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top