• HABARI MPYA

    Tuesday, May 28, 2013

    KUELEKEA TUZO ZA KILI KIKWETUKWETU 2013; KAVISHE AHIMIZA WANANCHI KUPIGIA KURA WANAMUZIKI DAKIKA ZA LALA SALAMA

    Pigeni Kura; Meneja wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe anahamasisha watu wapige kura kuchagua wanamuziki bora 2013 

    Na Princess Asia, IMEWEKWA MEI 28, 2013 SAA 1:40 MCHANA
    MENEJA wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager, wadhamini wakuu wa tuzo za Muziki Tanzania,  George Kavishe amewahimiza wapenzi wa muziki nchini kupiga kura kwa wingi kwa wasanii wanawaopenda waibuke washindi wa tuzo za mwaka huu.
    Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari leo mjini Dar es Salaam, Kavishe amesema tarehe ya mwisho ya kupiga kura hizo ni Mei 31, hivyo mashabiki watumie muda huu wa lala salama kupiga kura kwa wasanii wawapendao. 
    “Usije ukajilamu kwa vile haukupiga kura, una siku chache zilizobaki, piga kura kwa kutumia SMS, Email au mtandao wetu wa www.kilitimetz.com.  Vile vile nasisitiza kuwa makini katika upigaji kura ili kutopoteza kura yao. 
    “Hakikisha unatumia kodi sahihi ya msanii au kazi yake kwenye kura yako. Na kwa wale wa email msisahau kuhakiki kura yako, ukishatuma email system inatuma email yenye ‘link’ ya kubofya kuhakiki kura yako”. 
    Meneja huyo wa bia ya Kilimanjaro, aliongeza kuwa kwa kipindi chote tangu watangazwe wateule kwenye vinyang’anyiro mbali mbali kumekuwa na mapokeo tofauti. 
    “Naomba niahidi tena kwamba kila ushauri ama kukosolewa kwa tuzo hizi sie kwetu ni changamoto na tunapokea. Tunazoweza kurekebisha ama kujumuisha kwenye mchakato tunafanya hivyo. Yote ni kuhakikisha Tuzo hizi zinaendelea kukua katika ngazi ya kimataifa”. 
    Kavishe pia alimtambulisha kwa mara ya kwanza msemaji wa Academy kwa mwaka huu, Henry Mdimu na kuahidi kwamba kila mwaka kutakuwa na msemaji tofauti atakaechaguliwa na wana Academy wenyewe ili aweze kujibu maswali ama kutoa maelezo ya jinsi Academy inavyofanya kazi. 
    “Tunachojaribu kufanya ni kuweka uwazi zaidi kwa vile Academy inahusisha watu wenye uelewa mpana wa maswala ya muziki, mambo mengine yanayosemwa hawayakubali kwa vile wanajua kazi ya Academy ni ngumu na kamwe haiusishi rushwa wala upendeleo wa aina yeyote”. 
    Msemaji wa Academy alisisitiza kwama wana Academy huwa hawakutani kabla kupanga matokeo. “Tunaonana pale kwa mara ya kwanza na tunaingia moja kwa moja kwenye mchakato bila kupoteza muda. Tunazingatia vigezo vya uendeshaji ii kuleta ufanisi kwa zoezi zima.”
    Kavishe ameshukuru kwa kazi nzuri ya upigaji kura inyoendelea hadi sasa na kuwaomba wananchi wamalizie mchakato huu wa upigaji kura vizuri  katika siku chache zilizobaki.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: KUELEKEA TUZO ZA KILI KIKWETUKWETU 2013; KAVISHE AHIMIZA WANANCHI KUPIGIA KURA WANAMUZIKI DAKIKA ZA LALA SALAMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top