IMEWEKWA MEI 25, 2013 SAA 1:00 ASUBUHI
UWANJA wa Wembley leo utahimili vishindo vya Bayern Munich na Borussia Dortmund zote za Ujerumani katika Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Baada ya kuwasili London mapema jana, timu zote hizo zilipata fursa ya kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa timu ya taifa ya England, ambao utahimili vishindo vya fainali ya Ulaya kwa mara ya pili ndani ya miaka mitatu.
Dortmund imerejea katika fainali ya Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1997 walipoifunga Juventus ya Italia mabao 3-1 kwa msaada wa kocha wa Aston Villa, Paul Lambert, wakati Bayern inatumai kutwaa taji la tano la michuano hiyo baada ya kufungwa na Chelsea kwenye fainali mwaka jana.

Ugeni: Kocha wa Dortmund, Jurgen Klopp (kushoto) akiwa Wembley na kocha wa Aston Villa, Paul Lambert, ambaye aliiwezesha klabu hiyo ya Ujerumani kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa mwaka 1997

Mjadala mzito: Bastian Schweinsteiger, Arjen Robben na Franck Ribery wakiwa Wembley

Wachezaji wa Bayern Munich wakiingia Wembley kufanya mazoezi jana


Nyota: Robben (kushoto) na Ribery kati ya majina makubwa Wembley jioni ya leo

Anarekebishwa: Mshambuliaji tegemeo wa Dortmund, Robert Lewandowski akirekebishiwa viatu vyake

Kiatu cha mabao: Kiatu cha Lewandowski fainali

Utatu mtakatifu: Kevin Groskreutz, Robert Lewandowski na Marco Reus wakiwa mazoezini Wembley jana


.png)