• HABARI MPYA

    Friday, May 03, 2013

    MCHEZAJI SIMBA SC MAMBO YAMNYOOKEA ULAYA

    Ulaya safi; Emeh Izuchukwu

    Na Prince Akbar
    ALIYEWAHI kuwa mshambuliaji wa Simba SC, Mnigeria Emeh Goodwill Izuchukwu amejiunga na klabu ya Daraja la Pili Sweden, Elverum.
    Mpachika mabao huyo, aliyezaliwa Januari 9, mwaka 1992, amejiunga na timu hiyo ya Ligi ya Adecco akitokea klabu nyingine ya Sweden aliyoichezea hadi mwaka jana.
    Izuchukwu alitua Simba SC kwa pamoja na Mnigeria mwenzake, Orji Obinna mwaka 2008 na kucheza kwa misimu miwili kabla ya kuondoka kwa awamu.
    Ameporomoka; Tambwe Patiyo 'Diouf' 

    Wachezaji hao, walitolewa Simba SC kwa mkopo kutoka klabu ya Enyimba ya Nigeria na walionekana kufanya vizuri Msimbazi.
    Wakati Emeh aliuzwa Norway alikocheza hadi kuhamia Sweden, Obinna alishindana na Simba SC kwa sababu za kinidhamu.
    Mchezaji mwingine aliyewahi kucheza Simba SC kwa muda mfupi mwaka 2004, Patiyo Tambwe ‘Diouf’ ambaye alipata mafanikio makubwa Ulaya, kwa sasa ameshuka.
    Kijana huyo aliyezaliwa Januari 7, mwaka 1984 Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), alifikia hadi kusajiliwa na kuichezea FC Brussels ya Ubelgiji.
    Ameibuka; Odhiambo Blackberry

    Mshambuliaji huyo wa zamani wa DRC, Desemba mwaka jana alitemwa na klabu hiyo na kutimkia Thanh Hoa F.C. ya Vietnam.
    Naye kiungo aliyesajiliwa mwanzoni mwa msimu huu na kutemwa dirisha dogo Azam FC, George ‘Blackberry’ Odhiambo Ogutu amejiunga na Shirak FC ya Ligi Kuu ya Armenia, baada ya kuichezea kwa muda mfupi Nairobi City Stars.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MCHEZAJI SIMBA SC MAMBO YAMNYOOKEA ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top