![]() |
| Yakubu akishangilia kwa kuonyesha fulana yake ndani ya jezi inayomtakia heri kiungo Muamba aliyelazwa katika hospitalia ya London Chest |
KLABU ya Blackburn Rovers imejiondoa kwenye eneo la hatari
ya kushuka daraja katika Ligi Kuu baada
ya kushinda 2-0 dhidi ya Sunderland jana.
Junior Hoilett alifunga bao la kwanza dakika ya 58, akimtungua
kipa wa Sunderland, Simone Mignolet kabla ya Yakubu kuhitimisha ushindi wa Rovers
dakika nne kabla ya filimbi ya mwisho akiunganisha krosi ya Bradley Orr,
aliyetokea benchi.Blackburn inabaki nafasi ya 16 kwenye msimamo, ikiwazidi pointi sita Queens Park Rangers, Wigan Athletic na Wolverhampton Wanderers ambao wapo kwenye nafasi tatu za kuteremka daraja katika ligi hiyo ya timu 20.
Manchester City inayoshika nafasi ya pili, leo inaikaribisha Chelsea ikijaribu kupunguza pengo la pointi nne inazozidiwa na vinara na mabingwa watetezi, Manchester United wakati Tottenham Hotspur wanaoshika nafasi ya tatu wanaikaribisha Stoke City, Arsenal itasafiri hadi Everton na Liverpool itakuwa na kazi na QPR.
-celebrates120320R300.jpg)


.png)
0 comments:
Post a Comment