• HABARI MPYA

    Saturday, March 24, 2012

    NI VITA YA ADEBAYOR, DROGBA SPURS V CHELSEA LEO

    Drogba wa Chelsea
    Adebayor wa Chelsea
    MICKY Hazard amedai Tottenham wanatakiwa kuondoa hofu ya kumaliza juu ya Arsenal wakati watapoivaa Chelsea leo ili kutilia mkazo lengo lao la kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao.Kikosi Harry Redknapp kwa sasa kinashikiria nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi wakiwa nyuma kwa pointi moja kwa mahasimu wao wa kaskazini mwa London ikiwa imebakia michezo tisa kumalizika kwa msimu.
    Kuna wakati Spurs walikuwa mbele kwa pointi 10 kwa vijana wa Arsene Wenger, lakini wamekuwa na matokeo mabaya na kujikuta kwenye mazingira ya kutaka kukosa nafasi ya kucheza michuano hiyo mikubwa ya Ulaya.
    Safari bado inaendelea na jambo la msingi si kumaliza juu ya Arsenal, ila muhimu ni kucheza Ligi ya Mabingwa alisema Hazard
    “Mechi ya leo dhidi ya Chelsea ni kubwa nitakayotoa nafasi kwa Tottenham kumaliza katika tatu bora,” alisema Hazard. “Unapoangalia ratiba baada ya mechi ya Jumamosi, Spurs wanaratiba nyepesi kidogo.
    Arsenal ipo nafasi ya tatu baada ya kupata ushindi katika mechi nne mfululizo ambapo imeiengua Tottenham katika nafasi hiyo.
    Tottenham sasa inashika nafasi ya nne. Arsenal, yenye pointi 55, itaikaribisha Aston Villa wakati Tottenham yenye pointi 54, itakwaana na Chelsea inayoshika nafasi ya tano ikiwa na pointi 49, leo.
    Huko mkiani, Bolton itakuwa nyumbani kupambana na Blackburn. Timu hiyo haikucheza mechi ya katikati ya wiki dhidi ya  Aston Villa kufuatia wachezaji kukosa furaha baada ya Fabrice Muamba kuanguka uwanjani kwa matatizo ya moyo kwenye mechi dhidi ya Tottenham.
    Wakati kipute cha Ligi Kuu England kikifikia hatua tamu huku timu za mji mmoja Manchester City na Manchester United zikikimbizana kwa kasi kuwania ubingwa, Samir Nasri ameibuka na kujigamba kuwa Carlos Tevez ni silaha ya maangamizi.
    Tevez alionyesha kiwango kizuri katika mechi dhidi ya Chelsea, Jumatano wiki hii na Nasri anasema kuwa ataonyesha shughuli mpya katika mechi tisa za lala salama. 
    Alisema: “Tunafahamu anaweza kufanya nini katika kikosi."
    Mwanzoni mwa wiki hii kocha Alex Ferguson wa Man United, alikuwa akiomba dua baya ili Man City ifungwe na Chelsea, lakini kikosi cha Roberto Mancini kilishinda mabao 2-1.
    Tevez anatarajiwa kuishukia Stoke City kwenye mchezo wa ugenini leo  huku mashabiki wakiamini kuwa mbinu alizotumia dhidi ya Chelsea, zitaiua timu hiyo ambayo hutumia mabavu uwanjani.
    Manchester City haitakuwa na nyota kama Joleon Lescott, lakini Vincent Kompany anaweza kurudi uwanjani.
    Manchester United, ambayo imepata pointi 25 katika mechi tisa za karibuni, itakuwa na Phil Jones ambaye amepona mafua na Nani atarudi uwanjani baada ya kukosa mechi dhidi ya West Brom na Wolves.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NI VITA YA ADEBAYOR, DROGBA SPURS V CHELSEA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top