![]() |
| Setif wakiwa Uwanja wa Karume baada ya mazoezi juzi |
Alain alisema pia kuwa, mazoezi wanayofanya siyo kwa ajili ya kupambana na Simba tu, bali ni kusonga mbele kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho.
Kauli hiyo imekuja kufuatia kufanya mazoezi kwenye jua kali asubuhi na jioni.
Alisema kwa kawaida wao hufanya mazoezi kila siku asubuhi hata kama wana mechi siku hiyo, lakini kutokana na kutoizoea hali ya hewa ya Dar es Salaam, wameamua kufanya muda huo ili waweze kumudu kucheza.
"Tunafanya mazoezi wakati wa jua kali ili tuweze kuzowea baada ya kuona joto linatuchosha sana hivyo tusipojipanga tunaweza kukosa pumzi siku ya mechi yetu," alisema.
Simba na ES Setif zitashuka dimbani kesho katika mechi ya kwanza raundi ya pili kuwania Kombe la Shirikisho kwenye Uwanja wa Taifa.
Simba imepata nafasi hiyo baada ya kuindoa kwenye michuano Kiyovu ya Rwanda.



.png)
0 comments:
Post a Comment