LEO ni siku ya kufa na kupona kwa Manchester City wakati
watakapokuwa na kibarua cha kufufua matumaini yao ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu
ya England kwa kuvaana na Chelsea yenye ari mpya.
Wakiwa wanazidiwa pointi nne na vinara Manchester United na
mchezo mmoja mkononi, hakuna wepesi kuufikia ubingwa kwa City, ambao waliongoza
ligi hiyo mudea mrefu msimu huu.Chelsea ikiwa inawania nafasi ya tatu, baada ya kurudi kwenye hali nzuri, ikiwemo kufufua makali kwa mshambuliaji wake, Fernando Torres aliyeanza tena kufunga mabao, City wanatambua watakuwa na mechi ngumu kwenye Uwanja wa Etihad.
Ikizingatiwa kocha wa Man United, Sir Alex Ferguson aliiwezesha timu yake kushinda 5-0 dhidi ya Wolves Jumapili, kocha wa City, Roberto Mancini ana kazi ya ziada leo.
Mtaliano huyo anataka kumrejesha Carlos Tevez kwenye kikosi cha kwanza leo, baada ya Muargentina huyo kurejea kwenye timu.
Lakini kiungo wa City, Nigel de Jong anaamini timu hiyo inayotumia fedha nyingi inaweza kukabiliana na shinikizo.
"Hatuhofii upinzani na United," alisema Mholanzi huyo. "Hatuna woga wowote.
"Kwa siku 12 zilizopita tumekuwa kwenye wakati mgumu ambao hata wao hawakuupitia mwanzoni mwa msimu.
"Mechi 10 zilizobaki hizo ni fainali ya kuwania Kombe ¬ kwa sababu tupo kwenye ligi tu sasa."
City wanaingia kwenye mechi na Chelsea baada ya kutolewa Europa League na kipigo cha kushitua kutoka kwa Swansea kwenye mechi yao iliyopita ya Ligi Kuu.
Wanaweza kupigwa tafu na kurejea kwa Vincent Kompany, lakini watatakiwa kuwa makini na ‘kufufuka’ kwa Torres, ambaye alifuta gundu lake la kutofunga mabao kwa kutikisa nyavu mara mbili Jumapili.
Wakiwa wanazidiwa pointi nne na Tottenham na tatu na Arsenal, ushindi utafufua matumaini ya Chelsea kumaliza ligi ndani ya timu tatu za juu kwenye msimamo.
Tottenham itakuwa mwenyeji wa Stoke City leo, wakati Arsenal wataifuata Everton.
Liverpool, ipo nafasi ya saba ikizidiwa pointi 10 na Arsenal, lakini hawajapoteza matumaini yao ya kuwa ndani ya Top-Four na leo watakuwa ugenini na Queens Park Rangers.
Mechi kati ya Bolton na Aston Villa iliyokuwa ipigwe jana imeahirishwa kufuatia kiungo wa Bolton, Fabrice Muamba kuanguka na kupoteaza fahamu uwanjani Jumamosi kwenye mechi ya Kombe la FA na Tottenham na bado amelazwa katika hospitali ya London Chest akitibiwa moyo.
MECHI ZA LEO:
Tottenham v Stoke Man City v Chelsea
QPR v Liverpool
Everton v Arsenal



.png)
0 comments:
Post a Comment