• HABARI MPYA

    Monday, July 06, 2015

    MESSI, RONALDO NA WENGINE AMBAO WALIWIKA KATIKA KLABU, HAWAKUFANYA CHOCHOTE TIMU ZA TAIFA

    NI Lionel Messi mwenye pekee anajua kilichokuwa kwenye mawazo yake wakati mashabiki wadogo walipomfuata kuomba kupiga naye picha katikati ya Uwanja mjini Santiago, muda mfupi baada ya Argentina kushindwa kumaliza ukame wa mataji wa miaka 22.
    Kwa bahati mbaya, nyota huyo wa Barcelona, alisimama kupiga picha na kuwasainia hiyo ikiwa sehemu ya wajibu wake kama mchezaji mkubwa, hata baada ya ndodo zake kuyeyuka.
    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 anaweza assinue tena taji akiwa na timu yake ya taifa ya Argentina hadi anastaafu, tangu ashinde Medali ya Dhahabu ya Olimpiki mwaka 2008 China.
    Mshindi huyo mara nne wa Ballon d'Or si mchezaji pekee mkubwa ambaye alistaafu bila kushinda taji na timu yake ya taifa. Hapa, BIN ZUBEIRY SPORTS inakueletea wachezaji 10 wakubwa ambao hawajashinda mataji na timu zao taifa.
    Lionel Messi akiwa mnyonge baada ya Argentina kufungwa katika fainali na Chile kwa penalti 4-1 kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 120 

    Johan Cruyff, Uholanzi (1966-77: Mechi 48, mabao 33)
    Alishinda mataji mfululizo na klabu za Ajax, Barcelona na Feyenoord, lakini hakuna hata moja alilotwaa akiwa na jezi ya Uholanzi. Katika ngazi ya klabu, ameshinda mataji 10 ya Eredivisie na La Liga, na matatu ya Ulaya.
    Mafanikio makubwa kwa gwiji huyo kwenye soka ya kimataifa ni nafasi ya pili katika Kombe la Dunia Ujerumani mwaka 1974, taji ambalo lilichukuliwa na wenyeji na kushika nafasi ya tatu katika  Euro mwaka 1976Yugoslavia.
    Johan Cruyff alishinda mataji kibao akiwa na Ajax, Barcelona na Feyenoord, lakini hakushinda na Uholanzi
     
    Ferenc Puskas, Hungary (1945-55: Mechi 85, mabao 84), Hispania (1961-62: Mechi 4, hakufunga)
    Hungary ilitawala ulimwengu wa soka mwanzoni mwa miaka ya 1950. Puskas, kama Messi, alishinda Medali ya Dhahabu ya Olimpiki mwaka 1952, na hawakufungwa ndani ya miaka minne hadi wanafika katika Kombe la Dunia mwaka 1954.
    Walifika fainali, ambako Puskas alifunga bao la kuongoza licha ya kucheza amefungwa kichwani baada ya kupasuka.
    Hungary iliongoza 2-0, lakini mwishowe ikafungwa 3-2 na Ujerumani Magharibi. 
    Ferenc Puskas played for Hungary between 1945 and 1955, earning 85 caps and scoring 84 goals
    Ferenc Puskas aliichezea Hungary kati ya 1945 na 1955 mechi 85 na kufunga mabao 84
     
    Eusebio, Ureno (1961-73: Mechi 64, mabao 41)
    Mmoja kati ya wachezaji wakubwa kwa uwezo binafsi aliyeshinda mataji 11 na moja la Ulaya akiwa na Benfica.
    Mafanikio makubwa katika soka ya kimataifa kwa mshindi huyo wa Ballon d'Or 1965 ni mwaka 1966, alipoiwezesha Ureno kumaliza nafasi ya tatu Kombe la Dunia.
    Ureno kwa ujumla hawakuwa na timu bora ya kushinda Kombe hilo mwaka huo na Eusebio alijitolea kwa uwezo wake wote wote, lakini wapi!
    Eusebio alikuwa mmoja wachezaji bora mno wenye uwezo binafasi na akashinda mataji 11 na moja la Ulaya akiwa na Benfica

    Zico, Brazil (1976-86: Mechi 71, mabao 48)
    Tuzo binafasi alizoshinda Zico ni lukuki. Mshambuliaji huyo alikuwa mchezaji bora duniani mwishoni mwa miaka ya 1970 na mwanzoni mwa miaka ya 1980, ambayo Pele anakiri, lakini CV yake haijakamilika.
    Zico alishinda nafasi ya tatu katika Kombe la Dunia mwaka 1978 na akafika Robo Fainali mwaka 1986, lakini hakuwahi kutwaa taji.
    Zico alishinda nafasi ya tatu katika Kombe la Dunia mwaka 1978 na Robo Faibali mwaka 1986
     
    Paolo Maldini, Italia (1988-2002: Mechi 126, mabao 7)
    Maldini ameshinda mataji ya Serie A akiwa na AC Milan, pamoja na mataji matano ya Ulaya. Lakini anapokuwa na jezi ya Italia, beki huyo hana cha kujivunia.
    Nafasi ya pili katika Kombe la Dunia mwaka 1994 na Euro 2000, nafasi ya tatu katika Kombe la Dunia mwaka 1990, na Nusu Fainali Euro 1988 ndiyo mafanikio makubwa kwa Maldini kwenye soka ya kimataifa kabla ya kustaafu akiwa ana umri wa miaka 34 baada ya Kombe la Dunia mwaka 2002, miaka minne kabla ya Italia kutwaa taji hilo nchini Ujerumani mwaka 2006.
    Paolo Maldini won seven Serie A titles with AC Milan but could never win a major trophy for Italy
    Paolo Maldini ameshinda mataji saba ya Serie A akiwa na AC Milan, lakini hajashinda chochote na Italia
     
    Roberto Baggio, Italia (1988-2004: Mechi 56, mabao 27)
    Gwiji mwingine wa Italia, ambaye aliisaidia nchi yake kufika fainali ya Kombe la Dunia mwaka 1994 tena akiwa mfungaji bora wa mashindano.
    Baada ya sare ya 0-0 na Brazil ndani ya dakik 120, Baggio alikwenda kukosa penalti ya mwisho na akashindwa kutimiza ndoto za kubeba Kombe la Dunia.
    Roberto Baggio missed the final penalty of the 1994 World Cup that saw Brazil beat Italy for the trophy
    Roberto Baggio alikosa penalti ya mwisho katika Kombe la Dunia mwaka 1994 dhidi ya Brazil
     
    Michael Ballack, Ujerumani (1999-2010: Mechi 98, mabao 42)
    Ballack aliifikisha Ujerumani fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2002, lakini kadi ya njano aliyopewa kwa faulo ya kijanja aliyocheza katika Nusu Fainali dhidi ya Korea Kusini ilimfanya aukose mchezo wa fainali dhidi ya Brazil.
    Ujerumani ilifungwa 2-0 na Brazil. Alikuwepo kwenye kikosi cha Ujerumani kilichofika fainali Euro 2008 akiwa Nahodha wakifungwa na Hispania.
    Pamoja na kutamba akiwa na klabu za Bayer Leverkusen, Bayern Munich na Chelsea, lakini Ballack hakuwahi kutwaa taji akiwa na Ujerumani.
    Michael Ballack could not win a major trophy with Germany across his 11 years playing for his country
    Michael Ballack hakushinda taji lolote akiwa na Ujerumani licha ya kuichezea kwa miaka 11
     
    Paul Gascoigne, England (1988-98: Mechi 57, mabao 10)
    Kweli, unaweza kusema wakali wa England kama David Beckham, Steven Gerrard, Frank Lampard, Paul Scholes hawana nafasi hapa, lakini Gazza anastahili kuwamo kutokana na machozi aliyomwaga Italia '90.
    Ni huko ambako England ilimaliza katika nafasi ya nne na Gascoigne alimwaga machozi baada ya kuonyeshwa kadi ya njano dhidi ya Ujerumani Magharibi katika Nusu Fainali, maana yake angekosa fainali hata kama wameshinda. 
    Paul Gascoigne was reduced to tears at Italia '90 when England lost to West Germany in the semi-final
    Paul Gascoigne alimwaga machozi Italia '90 wakati England ikifungwa na Ujerumani Magharibi katika Nusu Fainali
     
    Michael Laudrup, Denmark (1982-98: Mechi 104, mabao 37)
    Wengi wanaamini Laudrup wa miaka 1990 ni kama Cruyff wa miaka ya 1970. Laudrup alikuwa nyota babu kubwa, aliyeshinda mataji na Juventus, Barcelona, Real Madrid na Ajax.
    Lakini hakuwa kushinda taji lolote na Denmark. Walifuzu kutoka Kundi E Kombe la Dunia mwaka 1986, lakini wakatolewa kwa kufungwa mabao 5-1 na Hispania katika raundi iliyofuata.
    Na wakati Denmark wanatwaa taji la Euro 1992, Laudrup alikuwa tayari amestaafu soka ya kimataifa waakti wa mechi za kufuzu. 
    Former Swansea City manager Michael Laudrup never won a major trophy with Denmark 
    Kocha wa zamani wa Swansea City, Michael Laudrup hakuwahi kushinda taji na Denmark 
    Brian Laudrup won Euro 1992 with Denmark but his brother Michael didn't take part in the tournament
    Brian Laudrup alishinda Euro 1992 akiwa na Denmark, lakini kaka yake, Michael hakucheza mashindano hayo
     
    Cristiano Ronaldo, Ureno (2003- hadi sasa: Mechi 120, mabao 55)
    Muda unayoyoma na akiwa na umri wa miaka 30 sasa, Cristiano Ronaldo anaelekea kustaafu soka ya kimataifa bila taji.
    Ronaldo hawezi hatasahau Euro 2004 ambayo Ugiriki iliifunga Ureno kutwaa taji hilo kama wenyeji. Je, kati yake na Messi katika umri wa miaka 30 na 28 mmoja wao au wote wanaweza kutimiza ndoto zao siku zijazo kabla ya kustaafu?
    Cristiano Ronaldo was stunned in the final of the Euro 2004 (pictured) when Greece beat Portugal
    Cristiano Ronaldo aliangulia kilio baada ya Ureno kufungwa na Ugiriki katika fainali ya Euro 2004
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MESSI, RONALDO NA WENGINE AMBAO WALIWIKA KATIKA KLABU, HAWAKUFANYA CHOCHOTE TIMU ZA TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top