KUNA uwezekano kuanzia msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara idadi ya wachezaji wa kigeni ikapanda hadi saba kuanzia msimu ujao.
Katika azimio la Bagamoyo miaka mitano iliyopita, ilikubaliwa kuanzia msimu uliopita idadi ya wachezaji wa kigeni ipunguzwe hadi kubaki watatu- na wakati huo ilipunguzwa kutoka 10 hadi watano.
Lakini mpango huo umeondoka na uongozi uliopita wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), chini ya Rais, Leodegar Tenga. Uongozi mpya wa TFF chini ya Rais Jamal Malinzi ulioingia madarakani Oktoba mwaka juzi, umeyumbishwa na shinikizo la klabu.
Kikao cha Kamati ya Utendaji wiki iliyopita kiliiagiza Kurugenzi ya Mashindano kufanyia uchambuzi maoni ya klabu juu ya idadi ya wachezaji wa kigeni yaliyowasilishwa hadi Mei 30, mwaka huu.
Baada ya kupitia maoni hayo ya klabu, Kurugenzi ya Ufundi itawasilisha maoni yake Kamati ya Mashindano, ambayo viongozi wake wakuu wanatoka kwenye klabu zinazoongoza kampeni ya nyongeza ya wachezaji wa kigeni.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ni Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ ambaye pia Makamu wa Rais wa Simba SC na Makamu wake ni Clement Sanga ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Yanga SC.
Kamati ya Mashindano ndiyo itakayowasilisha mapendekezo ya mwisho katika kikao kijacho cha Kamati ya Utendaji- ambayo itatoa uamuzi wa kukubali, au kukataa ongezeko la wachezaji wa kigeni.
Wazi kutokana na klabu kubwa, Azam FC, Simba SC na Yanga zinavyopambana kuhakikisha idadi ya wachezaji wa kigeni inaongezwa, kuna uwezekano msimu ujao klabu zikaruhusiwa kusajili wageni hadi saba kutoka watano kwa mujibu ya kanuni ya sasa.
Ni klabu tatu ndizo zinajua umuhimu wa kuwa na wachezaji wengi wa kigeni katika vikosi vyao, kati ya Klabu zote zaidi ya 30 za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara.
Klabu hizo, ni Azam FC, Simba SC na Yanga SC, zote za Dar es Salaam ambazo ndizo zimekuwa washindani wa ubingwa wa Ligi Kuu, inayodhaminiwa na Vodacom.
Kwa pamoja, Azam FC, Simba na Yanga SC zinaamini haziwezi kufanya vizuri katika michuano ya Afrika bila ya kuwa na wachezaji wengi wa kigeni, zikitazama timu nyingine zinazofanya vizuri huko mfano TP Mazembe ya DRC, zinaundwa na wachezaji wengi wa kigeni.
Kama DRC ni moja ya nchi zinazoaminika kuwa na wachezaji wenye vipaji na uwezo mkubwa wa kucheza soka, lakini klabu yake inayofanya vizuri katika michuano ya Afrika ina wachezaji zaidi ya 10 wa kigeni kikosini, vipi kwa Tanzania?
Bila shaka huo ndio mtazamo wa wababe wa soka ya nchi hii, Azam, Simba na Yanga SC- lakini ikumbukwe msimu wa 2008-2009 ilipitishwa kanuni ya kusajili wachezaji 10 katika Ligi Kuu na kuwatumia watano kwa wakati mmoja uwanjani, wakati kwenye michuano ya Afrika hakukuwa na kikomo.
Hata hivyo, Azimio la Bagamoyo mwaka 2007 lilipitisha kwamba kuanzia msimu uliopita idadi ya wachezaji wa kigeni kwa kila klabu iwe wachezaji watatu na kuanzia msimu wa 2009/2010 idadi ilipungua kutoka wachezaji 10 hadi watano.
Chini ya Tenga- TFF iliona klabu zimeshindwa kutumia vyema fursa ya kusajili wachezaji wengi wa kigeni, kwa kuleta wachezaji wenye uwezo mkubwa, badala yake waliletwa wachezaji ambao walikuwa wanazidiwa uwezo kwa mbali kabisa na wachezaji wa hapa.
TFF ikaona klabu hazijawa tayari kwa wachezaji wengi wa kigeni na kuamua kupunguza hadi kutoka 10 hadi watano- pia kutilia mkazo kwamba kuanzia msimu uliopita watabaki watatu.
Lakini TFF ya Malinzi sasa inaendelea na mchakato wa kuongeza wachezaji wa kigeni hadi saba.
Tulikwishapewa fursa ya kuwa na wachezaji 10 wa kigeni, lakini matokeo yake tukasajili wachezaji ambao hata kutuliza mpira hawajui- hadi TFF ikaamua kubadilisha kanuni hiyo.
Hilo ni jambo la msingi kutazama, lazima ufike wakati klabu ziache utaratibu wa kuletewa letewa wachezaji na mawakala, zifuatilie zenyewe wachezaji jambo ambalo ni rahisi.
Klabu lazima ziwe na vitengo maalum vya kufuatilia wachezaji, ambavyo watu wake watakuwa wanatazama Televisheni zinapochezwa mechi za Ligi za nje, Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho ili kutazama wachezaji wakali.
Rahisi tu, Televisheni ya SuperSport inaonyesha ligi nyingi za Afrika pamoja na michuano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho- huko watu wanaweza kupata wachezaji bora badala ya wale tuliokuwa tunaletewa akina Kanu Mbiyavanga na Jama Mba.
Lakini pia maskauti wa klabu wanaweza kwenda kwenye fainali za mashindano mbalimbali ya Afrika yakiwemo ya vijana, kusaka vijana wenye vipaji na kuleta ambao wataleta changamoto ya kweli kwenye soka yetu.
Tazama wale vijana wawili kutoka Ivory Coast, Kipre Tchetche na Kipre Balou- wote Azam FC iliwatoa katika timu ya vijana ya nchi hiyo iliyokuja kucheza michuano ya CECAFA Challenge mwaka 2010 hapa Dar es Salaam na wamethibitisha wao ni wachezaji kweli.
Didier Kavumbangu aliyenyakuliwa na Azam FC kutoka Yanga SC, alikuja hapa na klabu yake, Atletico ya Burundi na kwa kiasi fulani ameonyesha ni mchezaji wa ukweli- kama ilivyo kwa mwenzake Amisi Tambwe.
Tatizo huwa ni kwa hawa wachezaji wa kuletewa na mawakala, sijui akina Akuffo na Asamoah- ila kama zinafanyika taratibu nzuri za kutafuta wachezaji wazuri wa kigeni, nchi itafurahia kanuni hiyo. Ndiyo maana ninauliza, tunalilia wachezaji kibao wa kigeni, je sasa tuko tayari au tunafuata mkumbo tu? Alamsiki.

.png)
0 comments:
Post a Comment