KLABU ya AC Leopards ya Kongo imetinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika licha ya kufungwa mabao 3-1 leo na Warri Wolves ya Nigeria.
Lakini ushindi wa kwanza nyumbani wa mabao 3-0 mjini Dolisie umewasaidia Wakongo hao licha ya kipigo cha leo Uwanja wa Warri City.
Kipa wa Wolves, Daniel Akpeyi ndiye aliyekuwa shujaa leo baada ya kuokoa michomo mingi ya hatari ikiwemo ya Balkoua Carof na Ntela Kalema.
Katika mechi nyingine za leo, Hearts of Oak imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Esperance hivyo kutolewa kwa jumla ya mabao 5-1, baada ya awali kufungwa 4-0 Tunsia.
Orlando Pirates ya Afrika Kusini imeifunga 4-1 AS Kaloum na kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 4-3 baada ya awali kufungwa 2-0 mjini Bamako.
Mechi nyingine zinatarajiwa kuchezwa kesho Al Ahly wakiwa na mtaji wa ushindi mwembamba wa ushindi wa 2 - 1 watakuwa wageni wa Club Africain Tunisia, Sanga Balende wakiwa na mtaji mdogo wa 1-0 watakuwa wageni wa Zamalek, Sfaxien wakiwa na mtaji wa 2-0 watakuwa wageni wa Asec Mimosas, Raja Casablanca wakiwa na mtaji wa 2-0 watakuwa wageni wa ES Sahel na Stade Malien wakiwa na mtaji wa 2-0 pia watakuwa wageni wa AS Vita mjini Kinshasa.

.png)
0 comments:
Post a Comment