BARCELONA imetimiza ndoto za kutwaa mataji matatu, baada ya kuifunga mabao 3-1 Juventus ya Italia Uwanja wa Olimpiki mjini Berlin Ujerumani na kubeba Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya. Shukrani kwao wafungaji wa mabao hayo, Ivan Racitkic dakika ya nne, Luis Suarez dakika ya 68 na Neymar dakika ya 90, Barca ikirithi taji lililoachwa wazi na mahasimu wao, Real Madrid.
Bao pekee la Kibibi KIzee cha Turin lilifungwwa na Alvaro Morata dakika ya 55.
Barca ambayo tayari ina mataji ya La Liga na Kombe la Mfalme msimu huu, ingeondoka na ushindi mtamu zaidi, kama bao lingine la Neymar lisingekataliwa kwa madai aliunawa mpira kabla ya kufunga. Xavi alitokea benchi na kwenda kucheza mechi yake ya rekodi ya 151 ya Ligi ya Mabingwa akichukua nafasi ya Iniesta kipindi cha pili.
Kikosi cha Barcelona kilikuwa; Ter Stegen, Alves, Pique, Mascherano, Alba, Rakitic/Mathieu, Busquets, Iniesta/Xavi dk78, Messi, Suarez/Pedro dk90 na Neymar.
Juventus: Buffon, Lichtsteiner, Barzaglia, Bonucci, Evra/Coman dk89, Marchisio, Pirlo, Pogba, Vidal/Pereyra dk79, Tevez na Morata/Llorente dk85.
Safu hatari ya ushambuliaji ya watu watatu Barca; Luis Suarez, Messi na Neymar wakisherehekea na taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya PICHA ZAIDI GONGA HAPA


.png)
0 comments:
Post a Comment