Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
TANGU jana usiku kumekuwa na uvumi ambao chanzo chake haswa hakijulikani- kwamba mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi (pichani kushoto) anarejea Yanga SC.
Yanga SC haijasema chochote kwa muda wote huo, lakini Emmanuel Okwi mwenyewe leo ameandika kwenye akaunti yake ya Twitter kuzizima habari hizo.
Okwi ameandika kwa mchanganyiko wa lugha mbili, Kiingereza na Kiswahili; “Red and white all the way!! (Nyekundu na Nyeupe njia yote) Simba Sports Club Nguvu Moja,”.
Okwi yuko kwao Uganda mapumzikoni na hiki ni kipindi cha usajili kwa klabu za Tanzania. Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amezungumzia habari hizo akisema; “Ni porojo tu, Okwi ni wa Simba,”.
Yanga SC hawajasema chochote hadi sasa kuhusu hilo na uvumi umeendelea kuenezwa kwamba Mganda huyo yuko njia moja kurejea Jangwani.
Okwi alirejea Simba SC Agosti mwaka huu, baada ya kutemwa na Yanga SC iliyomsajili Desemba mwaka juzi kutoka SC Villa ya Uganda, ambayo nayo iliruhusiwa kumtumia na FIFA baada ya kuingia katika mgogoro na Etoile du Sahel ya Tunisia.
Okwi alijiunga na Etoile kwa dau la dola 300,000 za Kimarekani zaidi ya Sh. Milioni 600 akitokea Simba SC Januari mwaka 2014, lakini kufika Mei akatibuana na klabu hiyo.
Klabu ya Tunisia ilidai Okwi alipewa ruhusa ya kwenda kuchezea timu yake ya taifa, The Cranes akachelewa kurudi zaidi ya mwezi mzima, wakati mchezaji akadai alikuwa halipiwi mishahara.
Okwi na Etoile wakafunguliana kesi Shirikisho la Soka la Kimataia (FIFA) na mchezaji huyo wa Uganda akaomba aruhusiwe kuchezea timu nyingine kunusuru kipaji chake wakati sakata hilo linaendelea.
FIFA ikatoa ruhusa hiyo na Okwi akajiunga na klabu yake ya zamani, SC Villa ya Uganda lakini baada ya miezi sita, akasajiliwa na Yanga SC kwa Mkataba wa miaka miwili na nusu Desemba mwaka jana.
Hata hivyo, kufika Machi mwaka huu, Okwi akatibuana na Yanga SC na kuamua kuomba kurejea klabu yake, Simba SC ambako alifanikiwa. Yanga SC walifungua kesi TFF kupinga, lakini mshambuliaji huyo wa Uganda akawagaragaza na kupewa ridhaa ya kuendelea na kazi Simba SC, ambako alipewa Mkataba wa miezi sita.
Desemba mwaka jana ikaripotiwa kwamba Okwi amesaini Mkataba mpya na Simba wa miaka miwili, huku ule wa awali wa miezi sita ukielekea ukingoni.

.png)
0 comments:
Post a Comment