Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
IDADI ya wachezaji wa kigeni katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inaweza kupanda hadi saba kuanzia msimu ujao- tofauti na maazimio ya miaka mitano iliyopita kupunguza hadi kubaki watatu.
Katika azimio la Bagamoyo miaka mitano iliyopita, ilikubaliwa kuanzia msimu uliopita idadi ya wachezaji wa kigeni ipunguzwe hadi kubaki watatu- na wakati huo ilipunguzwa kutoka 10 hadi watano.
Lakini mpango huo umeondoka na uongozi uliopita wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), chini ya Rais, Leodegar Tenga. Uongozi mpya wa TFF chini ya Rais Jamal Malinzi ulioingia madarakani Oktoba mwaka juzi, umeyumbishwa na shinikizo la klabu.
Kikao cha Kamati ya Utendaji wiki iliyopita kiliiagiza Kurugenzi ya Mashindano kufanya uchambuzi wa maoni ya klabu juu ya idadi ya wachezaji wa kigeni yaliyowasilishwa hadi Mei 30, mwaka huu.
Baada ya kupitia maoni hayo ya klabu, Kurugenzi ya Ufundi itawasilisha maoni yake Kamati ya Mashindano, ambayo viongozi wake wakuu wanatoka kwenye klabu zinazoongoza kampeni ya nyongeza ya wachezaji wa kigeni.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ni Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ ambaye pia Makamu wa Rais wa Simba SC na Makamu wake ni Clement Sanga ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Yanga SC.
Kamati ya Mashindano ndiyo itakayowasilisha mapendekezo ya mwisho katika kikao kijacho cha Kamati ya Utendaji- ambayo itatoa uamuzi wa kukubali, au kukataa ongezeko la wachezaji wa kigeni.
Wazi kutokana na klabu kubwa, Azam FC, Simba SC na Yanga zinavyopambana kuhakikisha idadi ya wachezaji wa kigeni inaongezwa, kuna uwezekano msimu ujao klabu zikaruhusiwa kusajili wageni hadi saba kutoka watano kwa mujibu ya kanuni ya sasa.

.png)
0 comments:
Post a Comment