![]() |
| Kapata mshirika; Henry Joseph Shindika anang'ara Norway |
Na Boniface Wambura
SHIRIKISHO la Soka Norway (NFF) limetuma maombi ya kupatiwa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa mchezaji Mtanzania Godfrey Mlowoka ili aweze kucheza mpira nchini humo.
NFF inamuombea hati hiyo Mlowoka ili aweze kujiunga na klabu ya Ekne IL kama mchezaji wa ridhaa ambapo klabu yake ya zamani aliyokuwa akiichezea nchini imetajwa kuwa Sadani.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linafanyia kazi maombi hayo na mara taratibu zote zitakapokamilika hati hiyo ya uhamisho itatumwa nchini Norway.
Tayari Norway kuna mchezaji mmoja anayefanya vizuri katika klabu ya Kongsvinger ya Daraja la Kwanza, ambayo alijiunga nayo mwaka 2009 akitokea Simba SC.
Hadi sasa, Nahodha huyo wa zamani wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars amekwishaichezea timu hiyo mechi 74 na kuifungia mabao mawili.



.png)