• HABARI MPYA

    Thursday, October 25, 2012

    YUSSUF BAKHRESA WA AZAM AENDA HIJJA

    Yussuf Bakhresa

    Na Mahmoud Zubeiry
    WAKALA wa wachezaji anayetambuliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Yussuf Said Salim Bakhresa yupo, Makka, Saudi Arabia kwa ajili ya kufanya ibada ya Hijja kesho.
    Yussuf ambaye ni mtoto wa bilionea, Said Salim Bakhresa, mmiliki wa Azam FC, moja ya timu tishio katika Ligi Kuu nchini, anakuwa miongoni mwa vijana wachache wa Kitanzania waliothubutu kutekeleza nguzo hiyo ya tano ya Uislamu katika umri wa ujana.
    Alhaj huyo mtarajiwa anakuwa kiongozi wa pili kijana katika msafara wa Watanzania waliokwenda mwaka huu Hijja, baada ya Mwenyekiti wa Yanga, Yussuf Mehboob Manji.
    Yussuf Bakhresa pamoja na kuwa mtu muhimu katika ustawi wa Azam, lakini pia amekuwa mfano wa mawakala wa wachezaji hapa Tanzania waliofanya juhudi za makusudi kujaribu kuwatafutia timu Ulaya wachezaji nchini.
    Amewahi kumpeleka Mrisho Ngassa katika klabu ya West Ham United ya England ambako pamoja na kufuzu majaribio, akarudishwa Afrika ‘kuongeza lishe’. Amewahi kumpeleka John Bocco ‘Adebayor’ Israel ambako pia alikubalika mno.
    Yussuf pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Bakhresa Food Products Limited ingawa pia ni Mkurugenzi wa makampuni mengine yote ya Bakhresa, chini ya Mwenyekiti, baba yao, Said Salim Awadh Bakhresa.
    Wakurugenzi wengine wa Bakhresa Group Of Companies ni Mohamed, Abubakar na Omar. Mohamed ni Mkurugenzi Mtendaji wa Bakhresa Grain Milling (Uganda) na Mkurugenzi Mkuu wa Said Salim Bakhresa & Company Limited, wakati Omar ni Mkurugenzi Mtendaji Said Salim Bakhresa & Co Ltd na Abubakar Mkurugenzi Mkuu wa  Bakhresa Grain Milling (Malawi) na Bakhresa Grain Milling (Msumbiji) Limitad.
    Lakini pia Abubakar ni Mkurugenzi Mtendaji wa Said Salim Bakhresa & Co. Ltd na wote ni Wakurugenzi wa bodi ya Azam FC chini ya Mwenyekiti, mzee Said Salim Awadh Bakhresa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: YUSSUF BAKHRESA WA AZAM AENDA HIJJA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top