• HABARI MPYA

    Wednesday, October 24, 2012

    BIN ZUBEIRY YASHINDA TUZO YA COPA COCA COLA 2012

    Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Umma ya Coca Cola Kwanza, Evans Mlelwa (kulia), akimkabidhi Mahmoud Zubeiry aka BIN ZUBEIRY wa bongostaz.blogspot.com (kushoto) mfano wa Hundi ya Sh. Milioni 2, baada ya kushinda tuzo ya Mwandishi bora wa blogs wa mashindano ya Copa Coca Cola. Wengine katikati ni Meneja wa Sprite, Warda Kimaro na Katibu wa TASWA, Amir Mhando.

     KAMPUNI ya Coca Cola Kwanza, leo imewapa tuzo Waandishi watano wa Habari nchini, baada ya kuibuka vinara katika tuzo za Waandishi Bora wa mashindano ya soka ya vijana kwa umri chini ya miaka 17, Copa Coca Cola yaliyofanyika Julai mwaka huu.
    Upande wa Blogs, bongostaz.blogspot.com ya BIN ZUBEIRY imeibuka kinara na kuzawadiwa Sh, Milioni 2 sawa na washindi wengine, upande wa Televisheni, Jimmy Tara wa ITV, Radio, Amry Masare wa Radio One, Magazeti, Japhet Kazenga wa Daily News na Mpiga Picha, Mohamed Mambo wa Habari Leo.
    Tuzo hizo zilitolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Umma wa Coca Cola Kwanza, Evans Mlelwa, makao makuu wa kampuni hiyo ya vinywaji baridi, Mikocheni, Dar es Salaam.
    Mchakato wa kutafuta washindi uliendeshwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), ambacho leo kiliwakilishwa  na Katibu wake, Amir Mhando.

    Baadhi ya Waandishi waliohudhuria wakiwa kazini

    BIN ZUBEIRY anapokea mzigo

    BIN ZUBEIRY anapokea mzigo

    Washindi wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi 

    Washindi wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi 

    Jimmy Tara anapokea mzigo wake

    Amry Masare anapokea mzigo wake

    Kazenga ana[pokea mzigo wake

    Meneja wa Sprite, Warda Kimaro akizungumza na Waandishi wa Habari katika hafla fupi ya utoaji wa tuzo hizo, Mikocheni, Dar es Salaam, kulia ni Katibu wa TASWA, Amir Mhando na kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Umma ya Coca Cola Kwanza, Evans Mlelwa (kulia). 

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: BIN ZUBEIRY YASHINDA TUZO YA COPA COCA COLA 2012 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top