• HABARI MPYA

    Wednesday, October 24, 2012

    LIGI DARAJA LA KWANZA BARA YAANZA KUTIMUA VUMBI LEO

    Wachezaji wa Moro United wakimdhibiti mchezaji wa Simba (kushoto) katika mchezo wao wa kujipima nguvu kabla ya kuanza Ligi daraja la Kwanza wiki iliyopita. Moro inaanza na Villa Squad Mlandizi

    Na Prince Akbar
    LIG Daraja la Kwanza Tanzania Bara (FDL) inatarajiwa kuanza kutimua vumbi leo kwenye viwanja mbalimbali nchini.
    Kundi A kutakuwa na mechi tatu ambapo Burkina Faso itacheza na Mbeya City kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro wakati JKT Mlale itakuwa mwenyeji wa Small Kids kwenye Uwanja wa Majimaji, Songea.
    Nayo Kurugenzi itaumana na Majimaji katika Uwanja wa Wambi ulioko Mufindi mkoani Iringa. Kundi hilo litamaliza raundi ya kwanza keshokutwa (Oktoba 25 mwaka huu) kwa mchezo kati ya Mkamba Rangers na Polisi Iringa utakaofanyika Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
    Mechi za kundi B kwa leo ni Ndanda dhidi ya Transit Camp katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara na Villa Squad itakipiga na Moro United kwenye Uwanja wa Mabatini mjini Mlandizi. Oktoba 25 mwaka huu ni Green Warriors v Tessema (Mabatini, Mlandizi) na Polisi Dar v Ashanti United (Uwanja wa Chamazi).
    Kundi C leo ni Kanembwa FC v Polisi Dodoma (Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma), Mwadui v Morani (Kambarage, Shinyanga), Pamba vs Polisi Mara (Kirumba, Mwanza) na Rhino Rangers vs Polisi Tabora (Ali Hassan Mwinyi, Tabora).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: LIGI DARAJA LA KWANZA BARA YAANZA KUTIMUA VUMBI LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top