• HABARI MPYA

    Wednesday, October 31, 2012

    LIGI KUU YA VODACOM SASA KWENYE MTANDAO


    Dar es Salaam 25, Oktoba 2012….. Mdhamini  Mkuu wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania, imewekeza katika kuwawezesha mashabiki wa soka kupata taarifa na matukio ya mechi zote za ligi hiyo kupitia njia ya simu za kiganjani  na intanet.
    Kupitia mifumo mbalimbali ya kiteknolojia wateja wa Vodacom wataweza kupata matokeo ya mechi mbalimbali kupitia simu zao za kiganjani ukiwa na ujumbe mfupi wa maneno na mitandao ya kijamii.
    Akizungumzia hatua hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza, amesema, Mtandao wa Vodacom una miundombinu ya kutosha na unaongoza katika masuala ya teknolojia. Hivyo itatumika katika kuwawezesha mashabiki wa soka walioko ndani na nje ya nchi  kujua matukio mbalimbali ya ligi kuu ya Vodacom.
    “Licha ya ligi yetu kuonekana katika kituo cha Televisheni cha Super Sport. Tumejipanga sasa kuhakikisha inakuwa katika mitandao mbalimbali muda wote kwa kila mchezo na kila tukio katika soka, Mashabiki watapata taarifa za ligi popote watakapokuwa,” alisema Meza na Kuongeza kuwa, “Kupitia intanet  matukio haya yatapatikana kupitia Facebook na Twitter na mitandao mingine ya kijamii.”
    “Ili kupata matokeo na taarifa mbalimbali kupitia njia ya simu mteja wa Vodacom atatakiwa kupiga *149*01# kisha atachagua VODACOM FLAVA na akisha kujiunga na huduma hiyo itakayo muwezesha kupata taarifa na matokeo ya  mechi mbalimbali”
    Aliongeza kuwa, “ Kwa wateja wanaotumia facebook na twitter kwao ni rahisi zaidi kwani huduma hizo zinatolewa bure na Vodacom, hivyo mashabiki wa soka watatembelea Ukurasa wetu wa facebook na Twitter na kupata taarifa mbalimbali kuhusu ligi na wengine kujishindia zawadi kwa kujibu maswali mbalimbali zikiwemo tiketi za mechi za ligi,”
    Aidha Mkurugenzi huyo alitoa Pongezi kwa Vyombo vya habari kwa kazi kubwa inayofanya katika kuwahabarisha watanzania kuhusu michezo mbalimbali hususani ligi kuu ya Vodacom kupitia Televisheni, Radio, Magazeti na Mitandao ya kijamii.
    “Vyombo vya habari ni wadau wakubwa na wanafanya kazi nzuri sana katika kutoa taarifa hizi wanastahili pongezi, nasi tunaangalia namna ya kuwaunga mkono kwa namna moja ama nyingine katika jitihada za kukuza soka la Tanzania na tunaamini tutafika mbali.”
    Mkurugenzi huyo alihitimisha kwa kutoa pongezi kwa timu mbalimbali zinazoshiriki katika ligi kwa kusema kuwa zimeonesha hamasa kubwa na kubainisha kuwa ni ishara ya ukuaji wa soka katika soka la Tanzania ambalo ndio lengo kuu la Vodacom.
    “Ligi sasa imekuwa na msisimko kila timu inajitahidi kushinda kila mech,hadi sasa timu zote zimeonesha kiwango kikubwa na soka la kuvutia tunatarajia maendeleo haya yataleta tija hata kwa timu yetu ya Taifa kufanya vizuri. Vipaji vingi vinaonekana na ajira kwa vijana imeongezeka kupitia michezo,”  alihitimisha Meza.
    Kampuni ya Vodacom katika kuongeza msisimko kwa mashabiki wa ligi imetoa ofa mbalimbali msimu huu kwa kuwawezesha wateja wake kupata SMS 50, Muda wa maongezi wa dakika 30 na MB 50 kwa shilingi 400 Ili kuwasiliana na ndugu jamaa na marafiki. Pamoja na mambo mengine kampuni hiyo inaangalia namna ya kutoa adha ya ukataji tiketi kwa wateja wake kutumia huduma ya M - pesa kununua tiketi za mechi mbalimbali.
    Amir Maftah wa Simba katika mechi dhidi ya Coastal Union, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: LIGI KUU YA VODACOM SASA KWENYE MTANDAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top