BODI ya Viwanja vya Michezo (SSMB) imeifungia klabu ya Gor
Mahia kutumia viwanja vya Nyayo na Moi International Sports Centre Kasarani.
Hatua hiyo inakuja baada ya vurugu za mwishoni mwa wiki
katika mechi yao na wapinzani wao wa jadi, AFC Leopards ambayo ilivunjika baada
ya dakika 26 tu.
Uamuzi huo umefikiwa leo na kutangazwa na Mwenyekiti wa bodi,
Generali Mstaafu Daniel Opande.
Pamoja na hayo, uamuzi hao haupokewa vizuri na Gor Mahia ambayo
imechukuliwa kama ni wa haraka.
Kifungo
hicho kinawafanya Gor wawe na Uwanja mmoja tu wa kutumia, City ambao hauendani
na idadi kubwa ya mashabiki wao


.png)
0 comments:
Post a Comment