KUNDI la muziki wa
kizazi kipya la TMK Wanaume Family la jijini Dar es Salaam ni miongozi mwa
burudani zitakazokuwepo kwenye bonanza la vyombo vya habari linaloandaliwa na
Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA).
Bonanza hilo
litafanyika Machi 24 mwaka huu ukumbi wa
Msasani Beach Club, Dar es Salaam, huku TASWA ikiamini litakuwa bora na la
uhakika.
Licha ya Wanaume
Family, burudani nyingine itakuwa bendi
ya muziki wa dansi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’, ambapo wadhamini ni Kampuni
ya Bia Tanzania (TBL).
Tunataka bonanza
la mwaka huu liwe la aina yake kuanzia burudani, michezo na mambo mengine yawe
ya aina yake.
Bonanza litaanza
saa tatu asubuhi hadi saa mbili usiku, ambapo baadhi ya michezo
itakayoshindaniwa ni soka ya ufukweni, netiboli, wavu, mbio za magunia, mbio
meta 100, kuruka kichura, kuvuta kamba, kucheza muziki na michezo.
Mgeni rasmi katika
bonanza hilo atakuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ambaye pia ni
Mbunge wa Urambo Mashariki, Samuel Sitta.
Lengo la bonanza ni kuwaweka pamoja waandishi wote wa habari
bila kujali ni wa siasa, michezo, uchumi, afya na mambo mengine, ili
kubadilishana mawazo na kufurahi pamoja na huwa linafanyika mara moja kwa
mwaka, likiandaliwa na TASWA



.png)
0 comments:
Post a Comment